Pillay ataka wanawake na makundi madogo yapewe nafasi katika kutoa maamuzi

Kusikiliza /

Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ameshutumu kuendelea kutengwa kwa wanawake na makundi mengine madogo kukosa kushirikishwa kwenye masuala ya umma moja kwa moja au kupitia waakilishi wao.

Pillay amesema kuwa kuwatenga wanawake hakuwanyimi tu haki zao za binadamu lakini pia fursa ya kujenga maisha yao ya baadaye. Akiongea mjini Geneva wakati wa sherehe za mwaka huu za kuadhimisha siku ya kimataifa ya haki za binadamu Pillay anasema kuwa wanawake wanachukua asilimia 20 tu ya wabunge duniani ishara kwamba wana safari ndefu kabla ya kujumuika vilivyo katika utoaji wa maamuzi.

Makundi mengine mengi pia yanajikakamua kuweza kushiriki kwenye serikali na masuala mengine ya utunzaji wa sera. Wakati mwingine hata baada ya kufanywa jitihada kuhakikisha makundi hayatengwi kwenye usimamizi, ubaguzi bado imeshamiri na kuwa kuzungumkuti. Leo nawapongeza wale wote ambao wameteseka sana wakipigania kilicho chao na wale wote kwenye nchi zingine wanaosema " tuna usemi, tuna haki zetu na tunataka kushiriki kusimia jamii zetu na chumi zetu."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031