Nchi zenye wahamiaji zitambue athari za majanga na mizozo kwa wahamiaji: IOM

Kusikiliza /

wahamiaji

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji hii leo, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limetaka jumuiya ya kimataifa hususan nchi zinazotoa au kupokea wahamiaji kutambua athari za majanga na mizozo kwa wahamiaji.

Msemaji wa IOM Jean Phillip Chauzy ametolea mfano wahamiaji Laki Mbili nchini Libya kutoka nchi maskini ambao mwaka 2011 walijikuta katika mazingira ya mgogoro wa kisiasa, wakakosa ajira, pesa, nyaraka na hata mbinu ya kuwawezesha kurejea makwao kuungana na familia zao. Wahamiaji hao walipata hali mbaya hadi mashirika ya kimataifa yalipowarejesha makwao.

 

Bwana Chauzy amesema madhara hayo ya muda mfupi na muda wa kati yanapaswa kuzingatiwa kwa sababu mazingira ya mizozo na majanga huongeza machungu zaidi kwa wahamiaji ambao tayari wanaishi katika mazingira hatarishi na hivyo kuongeza mahitaji ya misaada ya kibinadamu.

(SAUTI CHAUZY)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930