Mkuu wa OCHA azuru Myanmar kupima mahitaji ya kibinadamu

Kusikiliza /

mahitaji ya kibinadamu,

Katika muktadha huo, mkuu wa Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos yuko nchini Myanmar kutathmini hali ya kibinadamu nchini humo pamoja na athari za mizozo kwenye majimbo ya Kachim na Shan Kaskazini ambayo yamewalazimu watu 75,000 kukimbia makwao tangu kuanza kwa mapigano mwaka 2011.

Amos pia atatathmini athari za ghasia za kikabila kwenye jimbo la Rakhine ambapo watu 115 walilazimika kuhama makawao. Bi Amos pia alitembelea kambi ya Jan Mai kwenye jimbo la Kachin yaliyo makao kwa wakimbzi wa ndani 700. Bi Amos ameelezea wasi wasi wake kutokana na hali ya watu waliolazimika kuhama makwao sehemu tofauti za nchi ambazo hazifikiwi na Umoja wa Mataifa. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA .

(SAUTI YA JENS LEARKE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031