Mkutano kuhusu chanjo ya watoto wafanyika Tanzania

Kusikiliza /

chanjo ya watoto

Wataalamun wa afya pamoja na watunga sera kutoka mataifa mbalimbali duniani pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wameanzisha mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kujadilia hali ya utoaji chanjo na namna ya kukabiliana na magonjwa yanayoweza kutibika kwa watoto.

Mkutano huo ambao umewajumuisha wajumbe zaidi ya 600, umehusisha Shirika la idadi ya watu UNFPA , na unafanyika chini ya kivuli cha fuko la kimataifa la chanjo na kinga yaani "Global Alliance for Vaccine and Immunisation (GAVI).

Mkataba wa hivi karibuni wa Umoja wa Mataifa unaotaka haki na usawa kwa maiasha ya watoto ni miongoni mwa maeneo yanayoangaziwa na wajumbe na shabaha iliyoko ni kuona kwamba yale yaliyofafanuliwa kwenye mkataba huo wa kimataifa yanatekelezwa kivitendo.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031