Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UM afanya mazungumzo na pande hasimu nchini Syria

Kusikiliza /

Leila Zerrougui

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya watoto na mizozo bi Leila Zerrougui amekamilisha ziara yake nchini Syria, ziara iliyomkutanisha na utawala wa nchi hiyo na makundi yaliyojihama na kujadili suala la usalama kwa watoto. Mjumbe huyo amesema kuwa kisa ambapo watoto wawili ya kipalestina waliuawa na kujeruhiwa kwenye kambi ya Al-Yarmouk mjini Damascus ni moja ya masaibu yanayowakumba watoto hasa nchini Syria.

Kwenye majadiliano yake na waakilishi wa seriakli Bi Zerrougui aliibua masuala ya mapigano na athari zake kwa watoto hasa matumizi ya silaha nzito na mashambulizi kwenye sehemu zenye watu wengi. Mwezi Aprili mwaka huu jeshi la Syria lilitajwa kwa mara ya kwanza kwenye orodha ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa kuwaua watoto na pia kwa kuendesha mashambulizi kwenye shule na hospitali.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031