Matumaini ya kuimarika sekta ya viwanda duniani, yayoyoma: UM

Kusikiliza /

viwanda

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imebainisha kuyoyoma kwa matumaini ya kukua kwa sekta ya viwanda duniani.

Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO limetoa takwimu za sekta ya viwanda kwa robo ya tatu ya mwaka huu ambazo zinaonyesha kuwa kiwango cha ukuaji kwenye sekta hiyo kilikuwa asilimia 2.2 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, kiwango ambacho ni cha chini zaidi tangu mwaka 2009.

UNIDO inasema ripoti hiyo inadhihirisha mkwamo mkubwa wa uchumi huko Ulaya na kudhoofika kwa harakati za kukuza uchumi huko Amerika Kaskazini na nchi za Asia Mashariki huku kwa nchi zinazoendelea kasi ya ukuaji uchumi imekuwa ndogo.

Ripoti hiyo pia inasema nchi zenye viwanda vingi zaidi duniani zikiwekwa katika kundi kwa ujumla zimekumbwa na mporomoko mkubwa wa uzalishaji, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2009.

Mathalani Ujerumani ilipata anguko kwa asilimia Moja nukat Saba, Uingereza asilimia Sifuri nukta Tisa, Ufaransa asilimia Moja nukta Tisa na Japani asilimia Nne nukta Sita

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031