Maafisa wa magereza wapokea mafunzo eneo la El Fasher

Kusikiliza /

maafisa wa magereza

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP , Muungano wa Afrika AU na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID wametoa mafunzo kwa maafisa wa magereza katika eneo la El Fasher kaskazini mwa jimbo la Darfur nchini Suadn kama moja ya njia ya kuboresha idara za sheria.

Mwakilishi wa UNAMID Hastings Amurani-Phiri amesisitiza kujitolea kwa ujumbe huo katika kushirikiana na idara za magereza kwenye mikakati ya kufikia viwango vya kimataifa. UNDP imefadhili ofisi ya kwanza ya aina yake eneo la El Fasher ofisi ambayo itaongoza na kuratibu huduma za kisheria kwa wafungwa. Kwa Ujumla maafisa 16 walikamilisha mafunzo ya miezi sita katika nyanja za useremala na ufundi wa magari na umeme. Maafisa hao watatoa mafunzo kwa wafungwa ambayo kwa manufaa yao siku zijazo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2014
T N T K J M P
« ago    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930