Kinyang'anyiro cha nafasi ya Mkurugenzi Mkuu WTO chaendelea: Kenya yampendekeza Amina Mohammed

Kusikiliza /

nembo ya WTO

Idadi ya majina ya watu waliopendekezwa kuchukua wadhifa wa Ukurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO pindi Mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy atakapomaliza muda wake mwakani yamezidi kuongezeka baada ya Kenya kumteua Balozi Amina Mohammed kuwania nafasi hiyo. Balozi Amina kwa sasani msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP.

Tayari mataifa mengine matano yameteua watu wao ambayo ni Mexico, Jordan, Costa Rica, New Zealand na Ghana.

Kwa mujibu wa taratibu za WTO, uteuzi wa majina utakoma tarehe 31 mwezi huu ambapo baraza kuu la shirika hilo litakutana tarehe 29 mwezi ujao kwa wagombea kujitambulisha.

Uchaguzi unapaswa kuwa umekamilika si zaidi ya tarehe 31 mwezi Mei mwakani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Septemba 2017
T N T K J M P
« ago    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
252627282930