Kamati ya UM juu ya haki za watoto yaalani kuendelea matukio ya kunyongwa watoto Yemen

Kusikiliza /

kunyongwa kwa watoto nchini Yemen

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto Jean Zermatten, amelaani na vikali tukio la kunyongwa kwa mtoto mmoja wa kike Hind Al-Barti akisema kuwa kitendo hicho kilichotekelezwa mwezi huu mjini Sana'a nchini Yemen ni ukiukwaji mkubwa wa mikataba ya Umoja wa Mataifa.

Duru zinasema kuwa mtoto huyo alikuwa na umri wa miaka 15 hivyo kupitishwa kwa adhabu ya kunyongwa ni kwenda kinyume na sheria za kimataifa ikiwemo mkataba wa kimataifa juu ya watoto. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031