IOM yapata msaada wa fedha za kujenga makazi ya dharura huko Kivu Kaskazini

Kusikiliza /

kambi nchini DRC

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limepokea dola Elfu 55 kutoka shirika la maendeleo la Uswisi, SDC kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa makazi ya dharura kwa watu 800 waliopoteza makazi yao huko Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kideomokrasi ya Congo, DRC.

Ujenzi wa makazi hayo unafuatia watu hao kukimbia makwao kutokana na vurugu zilizoibuka baada ya waasi wa kikundi cha M23 kuingia na kuchukua mji wa Goma tarehe 21 mwezi uliopita. Kukamilika kwa makazi hayo kutawezesha familia kuondoka katika majengo ya shule ambayo yalitumika kama hifadhi ya muda. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031