Imani ndiyo nguzo kuu ya utoaji ulinzi wa jamii ya wakimbizi: UNHCR

Kusikiliza /

nembo UNHCR

Zaidi ya watu 400 ikiwemo viongozi wa dini na wataalamu wa imani wamekusanyika mjini Geneva ambako wanajadiliana kuhusu tofauti za kiimani zinavyoweza kutoa mchango kuwasaidia watu wanaoandamwa na matatizo ikiwemo wakimbizi.

Mkutano huo wa siku mbili unashabaha ya kuangalia kwa kiasi gani pamoja na kuwepo kwa tofauti za kidini, lakini bado imani hizo zikawa katika nafasi nzuri ya kuwafikia kwa misaada ya kibinadamu mamia ya raia walioko kwenye maeneo yenye matatizo

Wakati akifungua kongamano hilo Kamishna wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi António Guterres, alisema kuwa licha ya kuwepo kwa tofauti za kiimani, lakini bado taasisi hizo zinawajibika kuwakimu watu walioko kwenye matatizo. Taarifa kamili na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031