Hali ya usalama Syria inatia wasiwasi, pande husika zifanye mashauriano: Brahimi

Kusikiliza /

Lakdhar Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za kiarabu, kwenye mgogoro wa Syria Lakdhar Brahimi, amesema hali nchini Syria bado inatia wasiwasi na hivyo ametaka pande husika kwenye mgogoro huo kuchukua hatua madhubuti kwa ustawi wa raia wa Syria.

Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yake na Rais wa Syria, Bashar Al Assad mjini Damascus.

Kuhusu mazungumzo yake na Rais Assad, Bwana Brahimi amesema ilikuwa ni heshima kubwa kwake kukutana na Rais Assad ambapo wote walizungumzia masuala kuhusu hatua zitakazochukuliwa siku za usoni.

Brahimi amesema kuwa Rais Assad alielezea hisia zake kufuataia hali ilivyo nchini Syria na pia kumfahamisha kuhusu mikutano aliyofanya na maafisa kutoka mataifa tofauti nje na ndani ya eneo hilo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031