Hali ya usalama huko Mali bado si nzuri: Ban

Kusikiliza /

Jeffrey Feltman

Baraza la Usalama leo limepatiwa taarifa ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu hali ya usalama ilivyo huko Mali Afrika Magharibi ambapo amesema hali ya usalama si nzuri na anaunga mkono mapendekezo ya Afrika kuhusu ulinzi na usalama nchini Mali.

Ripoti hiyo imewasilishwa na Msaidizi wa Bwana Ban kwa masuala ya kisiasa, Jeffery Feltman kwenye kikao cha baraza hilo mjini New York, Marekani.

Mapendekezo ya Bwana Ban ni pamoja na kuhakikisha uwepo wa ofisi ya kisiasa ya kisiasa kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako ambayo itawajibika kuwasiliana kila siku na na wadau wa Mali huku akisema kuwa jitihada zozote za kuleta amani nchini Mali zinapaswa kuhusisha raia wote wa Mali.

(SAUTI YA JEFFREY FELTMAN)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930