Hali ya tahadhari huko Sahel inazidi kujitokeza: Ban

Kusikiliza /

watoto, Sahel

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema hali ya tahadhari inazidi kujidhirisha kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika na hivyo ni muhimu hatua za haraka zikachukuliwa kukabiliana na hali hiyo.

Bwana Ban ametoa kauli hiyo leo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ambalo limekuwa na mjadala kuhusu amani na usalama barani Afrika, likijikita katika ukanda wa Sahel.

Amesema hatua ya wiki iliyopita ya baraza hilo kujadili hali ya usalama na amani Mali haitaweza kupata suluhu ya kudumu bila kushughulikia changamoto zinazokumba eneo zima la Sahel ambamo inapatikana nchi ya Mali.

"Mizozo ya kisiasa, ugaidi, usafirishaji wa madawa ya kulevya na biashara haramu ya silaha vinashamiri nje ya mipaka na kutishia amani na ulinzi. Hali mbaya ya hewa na uchumi dhaifu vinaongeza hatari zaidi kwa mazingira ya sasa. Mwaka huu pekee takribani watu Milioni 18 nukta Saba wameathiriwa na hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula. Over one million children under the age of five are at risk of acute malnutrition. Serikali na watu wa Sahel wanahitaji msaada wet. Umoja waMataifa umeshachangisha dola Bilioni Moja kusaidia nchi za ukanda huo kukidhi mahitaji ya wakazi wao."

Kwa upande wake Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko Sahel, Romano Prodi ameliezea baraza hilo kuwa ili kufanikisha lengo la kuleta amani eneo hilo, kuna umuhimu wa pande zote zinazoshughulikia mzozo huko Sahel kuwa na msimamo mmoja dhidi ya vitendo vyote vinavyokwamisha maendeleo ya amani kwenye eneo hilo ikiwemo ugaidi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031