Hakuna mtu anayestahili kutengwa katika kufurahia haki zake: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Wakati zimesalia siku chache tu kabla ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema hakuna mtu hata mmoja anayestahili kutengwa katika kufurahia haki zake, kama zilivyowekwa katika azimio la kimataifa la haki za binadamu.

Bi Pillay amesema kuwa mamilioni ya watu ambao wamekuwa wakijitoa mitaani kufanya maandamano katika miaka michache ilopita, ili kudai haki zao, na kutaka ikomeshwe hali ambapo serikali hufanya tu maamuzi bila kuwahusisha raia.

Bi Pillay amesema, kila mtu anafaa kuwa na sauti inayosikika, na kuhusishwa katika masuala ya kiuchumi na kisiasa, bila kujali jinsia, uwezo wa kimwili, dini, au mienendo ya kimapenzi:

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031