Ban azitaka serikali kuchukua hatua za dhati kuhusu ongezeko la joto duniani

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa serikali zilizo na uwakilishi kwenye kongamano la kimataifa la kuangazia mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCCC mjini Doha, Qatar, kudokeza mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukelezeka.

Bwana Ban amesema, kwanza, ameziomba ziafikie ahadi nyingine inayoandama mkataba wa Kyoto, ambao ndio ulio karibu sana na mkataba wa kimataifa kuhusu hali ya hewa.

Amezitaka pia zikubaliane kuhusu hatua za kudumu katika uwekezaji unaoambatana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema pia ni lazima taasisi ziwekwe kwenye miji ya Cancun, Mexico, na Durban, Afrika Kusini ili kusaidia kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika nchi zinazoendelea.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Natarajia serikali kudhihirisha kinagaubaga kuwa mazungumzo kuhusu chombo cha kimataifa, ambacho kinaheshimika kisheraia, yapo kwenye mkondo mzuri. Serikali zinapaswa kuonyesha kuwa zina hamu ya kuchukua hatua kuhusu pengo lililopo kati ya ahadi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya hewa na kinachotakiwa kuhakikisha joto duniani halipandi kwa zaidi ya nyuzi mbili.”

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031