Ban asema mwaka 2012 ulikuwa wa mizozo na migogoro

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa tathmini yake ya mwaka huu wa 2012 unaofikia ukingoni na kuelezea kuwa ulikuwa ni mwaka uliosheheni mizozo na migogoro lakini Umoja wa Mataifa licha ya hali hiyo uliweza kuendeleza ajenda yake ya maendeleo endelevu kwa karne ya 21 huku ikiendeleza jukumu lake la kulinda amani na utulivu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani, Bwana Ban ametaja migogoro kama vile nchini Syria, ukanda wa Sahel, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na rasi ya Korea kuwa ni mizozo iliyouweka Umoja wa Mataifa katika majaribu ya kusimamia misingi yake ya kusitisha migogoro na kujenga amani.

(SAUTI ya BAN)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031