Nyumbani » 28/12/2012 Entries posted on “Disemba 28th, 2012”

Sijasema Assad atakaa madarakani hadi 2014: Brahimi

Kusikiliza / Lakhdar Brahimi

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi Jumamosi atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Mosciw, ikiwa ni katika jitihada za kupatia suluhu mgogoro wa Syria. Taarifa hizo ni kwa mujib uwa msemaji wa Umoja wa [...]

28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Helikopta mbili za MONUSCO zashambuliwa huko GOMA

Kusikiliza / Helikopta ya MONUSCO

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, MONUSCO umesema helikopta zake mbili zilishambuliwa Jumatano usiku kaskazini mwa mji wa Goma. Taarifa ya MONUSCO inaeleza kuwa helikopta hizo zilikuwa katika safari zake za kawaida za kuthibitisha ubora wake wa kuruka ambapo moja ilishambuliwa huko Kibumba na nyingine Kanyamahoro, [...]

28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa wapitisha azimio la kupiga vita ukeketaji wa wanawake

Kusikiliza / Stop-FGM-480x268

Makala yetu wiki hii ambayo pia ni ya mwisho kwa mwaka huu wa 2012 inaangazia Azimio la aina yake lililopitishwa na Umoja wa Mataifa la kupiga vita ukeketaji wa wanawake. Harakati za kupiga vita ukeketaji wa wanawake, wasichana na watoto wa kike zinazidi kuzaa matunda. Na hatua ya hivi karibuni zaidi ni ile ya Baraza [...]

28/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan Kusini yajumuishwa rasmi orodha ya nchi maskini duniani: UNCTAD

Kusikiliza / Wananchi wa Sudan Kusini wakifurahia uhuru wa nchi yao.

Taifa la Sudan Kusini lililopata uhuru wake mwaka 2011 limejumuishwa rasmi katika orodha ya nchi maskini duniani na kufanya idadi ya nchi hizo kufikia 49. Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, limesema Sudan Kusini imejumuishwa tarehe 18 mwezi huu na hivyo ina haki ya kupata misamaha kadhaa ili iweze kuondokana na [...]

28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNDP yamkana mtu aliyedai kuwakilisha shirika hilo Ureno na Ulaya Kusini

Kusikiliza / nembo ya UNDP

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limesema halimtambui Artur Baptista da Silva, mtu ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni msemaji wake wa masuala ya Uchumi kwa Ureno na Ulaya Kusini. Taarifa ya UNDP imesema Da Silva siyo mtumishi wala hajawahi kuajiriwa na shirika hilo na kwamba maoni yoyote aliyotoa ni ya kwake [...]

28/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mafuriko Pakistani: Maelfu bado wahaha bila makazi ya kudumu

Kusikiliza / mafuriko Pakistan

Maelfu ya wananchi wa Pakistan ambao waliathiriwa na mafuriko ya mwezi wa Septemba bado hawajarejea kwenye maeneo yao ya awali. Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa idadi kubwa waathirika hao bado wanaendelea kusalia kwenye makambi na wengine kwenye mabanda kufuatia maeneo yao kuharibiwa vibaya na mafuriko. Kiasi cha watu milioni 4.8 wanaripotiwa kuathiriwa na mafuriko [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Teknolojia yatumika kurahisisha huduma kwa wakimbizi wa Sudan Kusini

Kusikiliza / mtoto wa wakimbizi

Teknolojia mpya na ya kisasa ndiyo iliyotajwa kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuyafikia mahitaji ya wakimbizi wengi wa Sudan Kusin. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, linatumia teknolojia mbalimbali ikiwemo mifumo ya satelite pamoja na mifumo mengine ya kiteknolojia kuwafikishia ujumbe wakimbizi hao. Pia shirika hilo linatumia teknolojia hiyo kutoa misaada ya [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yakamilisha utoaji wa misaada Mashariki mwa DRC

Kusikiliza / msaada nchini DRC, IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha oparesheni ya siku nne ya kuwagawia misaada isiyo chakula watu 6,500 waliohama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kati ya misaada iliyosambazwa kwenye eneo la Bulengo ni pamoja na matandiko ya kulalia, mablanketi, sabuni, vyombo vya jikoni na pia nguo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (SAUTI [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mengi yalitimizwa mwaka 2012: WHO

Kusikiliza / WHO

Shirika la afya duniani WHO limefanya tathmini ya kazi yake mwaka 2012 hasa jitihada za kukabiliana na magonjwa likisema kuwa mengi yalitimizwa mwaka huu ikiwemo kukomesha kusambaa kwa ugonjwa wa kupooza nchini India na kutimizwa kwa lengo la maendeleo ya Milenia la maji ya kunywa kabla ya muda wa mwisho. Taarifa kamili na Monica Morara. [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yasaidia waathirika wa vitendo vya Ubakaji huko Goma

Kusikiliza / wanawake nchini DRC

Kliniki ya muda iliyoanzishwa kwenye kambi ya Mugunga mjini Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC kwa ajili ya kusaidia wanawake waliokumbwa na visa vya ubakaji imeripotiwa kuwa mkombozi kwa makumi ya wanawake na wasichana waliokumbwa na mkasa huo. Afisa wa tiba katika kituo hicho Barubeta Maombi amesema msaada wanaotoa ni wa vipimo [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama latoa tamko juu ya hali ya usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Kusikiliza / baraza la usalama 1

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya hali ya Usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kushutumu vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa na kikundi cha waasi kiitwacho SELEKA kwenye miji mbali mbali nchini humo. Taarifa ya Baraza hilo imekariri wajumbe wake wakisema kuwa kitendo hicho kinakwamisha makubaliano ya amani ya [...]

28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930