Nyumbani » 24/12/2012
Entries posted on “Disemba 24th, 2012”
Kusikiliza /

Mtendaji Mkuu wa Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa biashara ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka, CITES, John Scanlon amesifu wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutaka uchunguzi dhidi ya madai kuwa waasi wa kikundi cha LRA wanaua tembo na kuuza meno yao kimagendo. Bwana Scanlon amesema hatua hiyo ni ya kihistoria [...]
24/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO Irina Bokova ameeleza kusikitishwa kwake na kubomolewa hivi karibuni kwa makaburi takribani matatu ya kihistoria katika mji wa Timbuktu nchini Mali. Taarifa ya UNESCO imemkariri Bi. Bokova akisema kitendo hicho kimetokea wakati shirika lake limeanza kutekeleza wajibu wake kwa wananchi wa [...]
24/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Miili ya askari wanne wa Urusi waliofariki dunia baada ya helikopta waliyokuwemo ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kutunguliwa huko jimbo la Jonglei siku ya Ijumaa imesafirishwa leo kwenda nyumbani. Ibada ya kuwaombea ilifanyika kwenye kituo cha UNMISS karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba. Naibu [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji, IOM hii leo limeanza tena mpango wa kuwarejesha makwao raia wa Sudan Kusini kutoka mjini Khartoum ambao maisha yao yako hatarini. IOM imesema raia hao wanaorejeshwa kwa ndege ni pamoja na wazee, wagonjwa na wengineo na mpango huo umeanza tena leo baada ya kusitishwa kufuatia kuanguka kwa ndege [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za kiarabu, kwenye mgogoro wa Syria Lakdhar Brahimi, amesema hali nchini Syria bado inatia wasiwasi na hivyo ametaka pande husika kwenye mgogoro huo kuchukua hatua madhubuti kwa ustawi wa raia wa Syria. Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake ukiwemo ukeketwaji na kusema kuwa vitendo kama hivyo vinaweka hatarini afya za wanawake na wasichana wengi kote duniani. Amesema afya za mamilioni ya wanawake na watoto duniani kote ziko hatarini na kwamba kuendelea kwa vitendo hivyo kunavunja haki zao za [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya majina ya watu waliopendekezwa kuchukua wadhifa wa Ukurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO pindi Mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy atakapomaliza muda wake mwakani yamezidi kuongezeka baada ya Kenya kumteua Balozi Amina Mohammed kuwania nafasi hiyo. Balozi Amina kwa sasani msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia Naibu [...]
24/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nchi za Asia – Pasific zimeridhia mpango wa utekelezaji unaotumia teknolojia ya anga za juu kushughulikia majanga ya kiasili na hatimaye kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwenye ukanda huo. Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa mkutano wa siku mbili ambapo mpango huo unataka tume ya Uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa nchi za Asia [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mamia ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamekosa makwao kutokana na machafuko yanayojiri katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo wameanza kupokea misaada muhimu ikiwemo vifaa vya kujikimu huku wasambazaji wa huduma hizo wakikabiliana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Kiasi cha familia 23,000 zilizoko jimbo la Kaskazini ya Kivu, kimepatiwa vifaa vya [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »