Nyumbani » 21/12/2012 Entries posted on “Disemba 21st, 2012”

Eritrea ionyeshe ushirikiano kushughulikia haki za binadamu: UM

Kusikiliza / eritrean-refugees

Mtaalamu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Eritrea Beedwantee Keetharuth ametaka nchi hiyo kuonyesha ushirikiano wa kushughulikia haki za binadamu nchini humo kwa mujibu wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imemkariri Bi. Keetharuth akisema [...]

21/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake

Kusikiliza / wanawake

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika. Mathalani ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, vipigo, uminyaji wa matiti ya watoto wa kike kama madai ya kumlinda mtoto dhidi ya kutumbukia kwenye ngono mapema na kadhalika. Moja mwa njia muafaka [...]

21/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jeshi la Sudan ladaiwa kufanya mashambulizi ya anga, raia wakimbia: UNAMID

Kusikiliza / UNAMID

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika unaolinda amani kwenye jimbo la Darfur, nchini Sudan UNAMID, umeeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za raia kukimbia makazi yao kutokana na mashambulio ya anga yanayodaiwa kufanywa na jeshi la Sudan na vikundi vyenye silaha huko Shangil Tobaya na Tawila kaskazini mwa Darfur. Taarifa [...]

21/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wakaribisha hatua ya Senegal ya kumfungulia mashtaka rais wa zamani wa chad Habre

Kusikiliza / ramani ya Senegal

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha hatua ya bunge la Senegal ya kupitisha sheria ya kubuniwa kwa sehemu ya mahakama itakayoendesha kesi dhidi ya rais wa zamani wa Chad Hissene Habre. Ofisi hiyo inasema kuwa imekuwa ikiunga mkono jitihada za Muungano wa Afrika AU za kuhakikisha kuwepo uwajibikaji kufuatia ukiukaji wa [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kurejelea usambazaji wa chakula kwa watoto wanaotaabika nchini Swaziland

Kusikiliza / watoto nchini Swaziland

Shirika chakula la Umoja wa Mataifa WFP litarejelea shughuli za usambazaji wa chakula kwa vituo 1600 vya huduma nchini Swaziland baada ya shughuli hiyo kuvurugwa mapema mwaka huu kutokana na ukosefu wa ufadhili. Kulingana na WFP usambazaji huo wa chakula utawanufaisha mayatima 97,000 na watoto wengine 33,000 wanaotaabika. Asilimia kubwa ya watakaopokea chakula hicho ni [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakazi wa Haiti waishio kambini bado wakumbwa na madhila makubwa: IOM

Kusikiliza / kambi nchini Haiti

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la uhamiaji duniani, IOM pamoja na mashirika yake imeonyesha madhila ambayo bado yanawakumba wakazi wa Haiti kufuatia majanga ya mfululizo yaliyokumba nchi hiyo kuanzia mwaka 2010. Mathalani ripoti hiyo inaonyesha ukosefu wa ajira, watu kuendelea kuishi kwenye makazi na idadi kubwa ya kaya kuongozwa na wanawake pekee. Tupate taarifa zaidi [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wanajeshi wa DRC na waasi washutumiwa kwa kuhusika kwenye vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu

Kusikiliza / kikundi cha waasi cha M23, Goma

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kulingana na uchunguzi lililoendesha limebainisha kuwa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na wapiganaji wa kundi la M23 walitekeleza vitendo vinavyokiuka haki za binadamu wakati wa mapigano ya kutaka kuudhibiti mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo. Vitendo hivyo vinaripotiwa kutekelezwa kati ya tarehe 20 na 30 [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zisibugudhiwe wakati wa migogoro: WHO

Kusikiliza / nembo ya WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema shambulio lolote dhidi ya wahudumu wa afya halikubaliki na kwamba migogoro au mapigano yoyote hayapaswi kubughudhi huduma za afya. WHO imetoa kauli hiyo kufuatia kupigwa risasi na kuuawa kwa wafanyakazi sita waliokuwa wanaendesha kampeni ya polisi nchini Pakistan. Shirika hilo limesema vitendo hivyo vikifanyika, wanaopata madhara ni watoto na [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kutoa mgao wa dharura wa chakula huko Yarmouk: Yahitaji fedha zaidi

Kusikiliza / kambi ya Yarmouk

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP litaanza kusambaza msaada wa dharura wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa kipalestina waliokumbwa na mapigano kwenye kambi ya Yarmouk, iliyoko mji mkuu wa Syria, Damascus. WFP inatarajia kuwapatia msaada huo ambao ni mlo wakimbizi 125,000 wa kipalestina pamoja na raia wa Syria waliokimbia makazi [...]

21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031