Nyumbani » 20/12/2012 Entries posted on “Disemba 20th, 2012”

Waasi Mali vunjeni uhusiano na vikundi vya kigaidi: Azimio Baraza la Usalama la UM

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Kwa kutambua athari za mzozo wa mali kwa amani na usalama duniani, hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio ambalo pamoja na mambo mengine linataka waasi nchini humo kuvunja mara moja uhusiano na vikundi vya kigaidi ikiwemo Al-Qaida na kuthibitisha hatua hiyo. Azimio hilo pia linataka mamlaka za [...]

20/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNAMID yapata kiongozi mpya: Ni Mohamed Ibn Chambas

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Mkuu mpya wa UNAMID Mohamed Ibn Chambas

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wamemtangaza Mohamed Ibn Chambas kuwa kiongozi mpya wa UNAMID ambao ni ujumbe wa pamoja wa pande mbili hizo wa kulinda amani kwenye jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur. Bwana Chambas ambaye ni raia wa Ghana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ibrahim Gambari ambaye Katibu Mkuu wa Umoja wa [...]

20/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Dhuluma ya kingono imekithiri Jamhuri ya Afrika ya Kati: Bangura

Kusikiliza / Zainab Hawa Bangura

  Wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wamezingirwa na mzozo na kujikuta wakikumbwa na vitendo vya dhuluma ikiwemo kubakwa wamesema wamechoshwa na hali hiyo na sasa wanataka amani na wenzao wanaoshikiliwa na waasi waachiwe huru. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya ukatili wa ngono kwenye mizozo, Zainab [...]

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Makao makuu ya serikali ya mtaa yaibua mzozo Sudan Kusini, Wanawake na watoto wakimbia: UNMISS

Kusikiliza /

Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kimesema hivi sasa kinatoa hifadhi kwa raia wengi wao wanawake na watoto ambao wamekimbia mji wa WAU ulioko jimbo la Bahr el-Ghazal kutokana na mzozo juu ya makao makuu ya serikali ya mtaa. Jason Nyakundi ameandaa taarifa kamili. (SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wapalestina 100,000 waikimbia Syria

Kusikiliza / Mkimbizi wa kipalestina

  Maelfu ya wapalestina kwa sasa wanaendelea kuihama Syria kufuatia kuwepo mapigano makali yaliyotokea kwenye kambi ya Yarmouk mjini Damascus. Kambi hiyo ilishambuliwa kwa mabomu na ndege za kivita za Syria siku ya Jumapili kufuata tuhuma za kuwepo kwa waasi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestinba UNRWA linakadiria kuwa theluthi mbili [...]

20/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama la UM lalaani mashambulizi huko Jamhuri ya Afrika ya kati

Kusikiliza / Nyumba zilizobomolewa kutokana na mashambulio kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yaliyoendeshwa na  makundi yaliyojihami siku chache zilizopita kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya kati pamoja na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaondelea. Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari wajumbe wa Baraza hilo pia wameelezea wasiwasi wao kutokana na hali ilivyo nchini humo [...]

20/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watu 55 wafa maji huko Somalia: UNHCR

Kusikiliza / boat-300x214

Watu hamsini na watano wakiwemo raia wa Somalia na Ethiopia wanahofiwa kufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kando mwa pwani ya Somalia siku ya Jumanne. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema maiti 23 wamepatikana na watu wengine 32 bado hawajulikani walipo kwa hiyo inaaminika wamezama. Watu hao walikuwa wakisafiri kwa [...]

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maendeleo dhahiri yamepatikana katika ujenzi wa amani: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon akihutubia Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ujenzi wa amani baada ya migogoro ambapo Katibu Mkuu Ban Ki- Moon amesema maendeleo ya dhati yamepatikana katika ajenda ya ujenzi wa amani. Akihutubia kikao hicho, Bwana Ban amesema hata licha ya mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto lukuki. Amesema baadhi [...]

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR yaomba Kenya iendelee kulinda haki za wakimbizi

Kusikiliza / Makambi ya wakimbizi Dadaab Kenya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na matukio ya hivi karibuni nchini Kenya ya kuuawa kwa raia pamoja na wakimbizi. UNHCR imesema inalaani mashambulizi hayo na kutoa rambirambi kwa waathirika wote, watu na serikali ya Kenya huku ikiomba serikali hiyo kuendelea kulinda haki za wakimbizi.

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwegemeo wa imani za kidini wadhihirika katika mapigano nchini Syria: Tume huru

Kusikiliza / shelling-homs-syria-300x257

Mgogoro unaoendelea nchini Syria umeripotiwa kuchukua mwelekeo wa kidini ambapo baadhi ya vikundi vinalazimika kupambana ili kujilinda au kuonyesha mshikamano na moja ya pande zinazozozana katika mgogoro huo. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Tume huru iliyoundwa kuchunguza mzozo wa Syria ambapo imesema majeshi ya serikali na wanamgambo wenye silaha wamekuwa wakishambulia raia wa madhehebu [...]

20/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

ICTR yamhukumu Waziri wa zamani wa Rwanda kifungo cha miaka 35 jela

Kusikiliza / Augustin Ngirabatware

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Rwanda, imemhukumu waziri wa zamani wa nchi hiyo Augustin Ngirabatware kifungo cha miaka 35 jela baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na mauaji ya halaiki nchini mwake mwaka 1994. Akisoma hukumu hiyo, Jaji William Hussein aliyeongoza jopo la majaji watatu amesema Ngirabatware amepatikana na hatia ya [...]

20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mshikamano ni suluhu ya kutatua migogoro inayokumba dunia: Ban

Kusikiliza / Siku ya kimataifa ya mshikamano baina ya binadamu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya mshikamano kibinadamu hii leo na kusema mshikamano ndio njia pekee ya kutatua migogoro inayokumba dunia ya sasa yenye mwingiliano mkubwa. Ujumbe wa mwaka huu ni ubia wa kimataifa kwa ustawi wa pamoja. Amesema siku hii ni muhimu zaidi kwa [...]

20/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031