Nyumbani » 19/12/2012 Entries posted on “Disemba 19th, 2012”

Usalama kambi ya Mugunga huko Goma si nzuri: Wanawake wapaza sauti zao

Kusikiliza / kambi ya Mugunga, Goma

Umoja mataifa kupitia msimamizi Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous umetangaza bayana kuwepo kwa sintofahamu ya hali ya usalama huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Hali hiyo imeibuka baada ya kuondoka kwa waasi wa M23 mwanzoni mwa mwezi huu, lakini kumeripotiwa [...]

19/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ampongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea

Kusikiliza / Rais mteule wa Jamhuri ya Korea Park Geun-hye

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemtumia salamu za pongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea na kuelezea utayari wa kushirikiana na serikali mpya ya nchi hiyo. Bi. Park, mtoto wa dikteta wa zamani nchini Jamhuri ya Korea Park Chung-hee,  ameibuka mshidni katika uchaguzi wa Jumatano na anakuwa [...]

19/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka kurejeshwa haraka kwa mchakato wa amani kati ya Israeli na Palestina

Kusikiliza / Watoto wakicheza katika mabaki ya  uwanja wa mpira huko Gaza

Wito wa kutaka kurejeshwa kwa haraka mchakato wa amani kati ya Palestina na Israeli umetolewa kwa nyakati tofauti hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, kutokana na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande mbili hizo kufanyika mara ya mwisho mwezi Septemba mwaka 2010. Katika mkutano wake wa [...]

19/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watafuta fedha zaidi kukabiliana na waasi wa LRA

Kusikiliza / waasi wa  LRA

Katika harakati za kukabiliana na vitendo viovu vinavyofanywa na kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army kwenye maeneo ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinatafuta fedha zaidi kutekeleza mipango yake ya kudhibiti kikundi hicho. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Ya [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asema mwaka 2012 ulikuwa wa mizozo na migogoro

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa tathmini yake ya mwaka huu wa 2012 unaofikia ukingoni na kuelezea kuwa ulikuwa ni mwaka uliosheheni mizozo na migogoro lakini Umoja wa Mataifa licha ya hali hiyo uliweza kuendeleza ajenda yake ya maendeleo endelevu kwa karne ya 21 huku ikiendeleza jukumu lake la kulinda amani na [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

MONUSCO imejiandaa kwa lolote: Hervé Ladsous

Kusikiliza / Herve-Ladsous

Tangu kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka mji wa Goma mapema mwezi huu, hali ya sintofahamu kuhusu usalama kwenye eneo hilo imeendelea kudumu katika mji huo mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini. Kutokana na hali hiyo Msimamizi Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwa Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema MONUSCO ambacho [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maafisa wa magereza wapokea mafunzo eneo la El Fasher

Kusikiliza / maafisa wa magereza

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP , Muungano wa Afrika AU na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID wametoa mafunzo kwa maafisa wa magereza katika eneo la El Fasher kaskazini mwa jimbo la Darfur nchini Suadn kama moja ya njia ya kuboresha idara za sheria. Mwakilishi wa UNAMID Hastings [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNECE yaidhinisha mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani

Kusikiliza / nembo ya UNECE

Mkataba wa kimataifa wa matumizi ya vito vizito umepiga hatua baada ya kuungwa mkono na mataifa kadhaa kufuatia jitihada za majadiliano za miaka 3. Mkataba huo ambao ni umeratibiwa na kamishna ya kitaifa inayohusika na masuala ya uchumi barani Ulaya UNECE umelenga kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani. Kwa mara ya kwanza mkataba huo uliasisiwa [...]

19/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UM na mashirika ya kibinadamu yatoa ombi la msaaada kwa taifa la Haiti

Kusikiliza / Nigel Fisher

Umoja wa Mataifa na washirika wa huduma za kibinadamu wametoa ombi la dola milioni 144 zitakazotumika kusaidia zaidi ya watu milioni moja nchini Haiti mwaka 2013. Ufadhili huo utayawezesha mashirika ya kutoka misaada kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula, ugonjwa wa kipindupindu na hamiaji kwenye taifa hilo la Caribbean. Mratibu wa huduma za kibinadamu [...]

19/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukiukaji wa haki za binadamu bado ni changamoto nchini Iraq: UM

Kusikiliza / waandamanaji nchini Iraq

Suala la haki za binadamu nchini Iraq bado limesalia kuwa changamoto wakati taifa hilo linaposhuhudia mabadiliko kutoka nyakati zilizokuwa na mizozo na ghasia ikielekea kwenye demokrasia na amani imesema ripoti kuhusu haki za binadamu ya shirika la Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo inasema kuwa suala la ghasia limesalia ajenda kuu huku idadi ya raia waliouawa [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Syria wazidi kuongezeka: UM waomba dola Bilioni 1.5 kusaidia wakimbizi

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Idadi ya raia wa Syria waliopoteza makazi yao kutokanana mapigano yanayoendelea nchini mwao inatarajiwa kuongezeka na kufikia Milioni Nne katika nusu ya kwanza ya mwaka ujao. Umoja wa Mataifa unasema kuwa kati yao, Milioni Moja watakuwa wamekimbilia Jordan, Uturuki, Lebanon, Misri na idadi ya wakimbizi wa ndani itafikia Milioni Mbili. Kwa mantiki hiyo basi Umoja [...]

19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031