Nyumbani » 18/12/2012 Entries posted on “Disemba 18th, 2012”

Dunia hatarini kutumbukia katika mdororo mpya wa uchumi: Ripoti UM

Kusikiliza / Robert Voss

Ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2012 umedorora kiasi na hali hiyo inatarajiwa kuaendelea kwa miaka miwili ijayo, na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo. Rob Vos, ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya sera na upembuzi ya Umoja wa Mataifa amesema uchumi wa dunia [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uamuzi wa Baraza Kuu la UM wa kuanzisha siku ya kimataifa ya Radio wapongezwa

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne tarehe 18 Disemba limeridhia tarehe 13 ya mwezi Februari kila mwaka kuwa siku ya Radio duniani, ikiwa ni kutambua mchango wa Radio katika kurusha matangazo mbali mbali ya kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na vile vile kwa kutambua nafasi ya Radio ya Umoja wa [...]

18/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu laridhia tarehe 13 Februari kuwa siku ya Radio duniani

Kusikiliza / katika kuadhimisha siku ya radio

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limeridhia azimio la shirika   la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO la kutaka tarehe 13 Februari ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Radio duniani. Tarehe 13 Februari mwaka 1946 ni siku ambayo Radio ya Umoja wa Mataifa ilianza kufanya kazi ambapo Baraza [...]

18/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa UM afanya mazungumzo na pande hasimu nchini Syria

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya watoto na mizozo bi Leila Zerrougui amekamilisha ziara yake nchini Syria, ziara iliyomkutanisha na utawala wa nchi hiyo na makundi yaliyojihama na kujadili suala la usalama kwa watoto. Mjumbe huyo amesema kuwa kisa ambapo watoto wawili ya kipalestina waliuawa na kujeruhiwa kwenye kambi [...]

18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wengi wayakimbia machafuko Misri, UNRWA yakabiliwa na mzigo wa wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / watoto nchini Syria

Kumekuwa na hali ya mkwamo unaowaandama raia wa Syria katika wakati ambapo matokeo ya mzozo huo umeathiri pia ustawi jumla ya wale wanaotajwa wakimbizi wa Kipalestina. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa Palestina UNRWA, limeanzisha juhudi ya usambazaji wa huduma za kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi 150,000 walioko katika kambi ya Yarmouk. [...]

18/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uzalishaji wa mazao ya misitu bado ni wa kusuasua tangu kutokea anguko la uchumi wa dunia

Kusikiliza / uzalishaji wa mazao ya misitu

  Uzalishaji wa mazao yatokanayo na misitu unaarifiwa kusuasua tangu kushuhudiwa kwa mkwamo wa uchumi wa dunia, huku mataifa yaliyoko katika kanda ya Asia-Pacific ndiyo yakishika nafasi ya kwanza. Hata hivyo China ndiyo iliyotajwa kuwa ndiyo inayofanya vizuri zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani. Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO [...]

18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kampuni binafsi za ulinzi nchini Somalia ziongozwe kwa kanuni na sheria : Wataalamu UM

Kusikiliza / Faiza Patel

Wakati Somalia inajenga upya taasisi zake za ulinzi na usalama, serikali ya nchi hiyo imetakiwa kuhakikisha kuwa vikosi binafsi vya ulinzi vinaongozwa kwa kanuni na sheria na havigeuzwi kuwa mbadala wa vikosi thabiti vya polisi. Hilo ni tamko lililotolewa na kikundi cha wataalamu wanaochunguza matumizi ya mamluki waliofanya ziara nchini Somalia kwa siku saba wakiongozwa [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu nchini Syria yazidi kuzorota

Kusikiliza / mama na mtoto nchini, Syria

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kuzorota ambapo mahitaji ya chakula yanazidi kuongezeka, halikadhalika idadi ya watu wanaopoteza makazi yao. Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa hivi sasa wanahudumia watu Milioni Moja na Nusu kwa mwezi nchini Syria. Hata hivyo [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita DRC Mathiew Ngudjolo Chui hana hatia: ICC

Kusikiliza / Mathieu Ngodjolo Chui, ICC

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC imeamuru kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu, Mathieu Ngudjolo Chui baada ya kumuona kuwa hana hatia. Uamuzi huo umepitishwa kwa kauli moja na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Bruno Cotte kutoka Ufaransa ambapo wamesema upande wa mashtaka umeshindwa [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukosefu wa usalama mjini Goma wahatarisha maisha ya wakimbizi wa ndani

Kusikiliza / wahamiaji wa ndani, DRC

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya usalama kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mugunga 3 karibu na mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemeokrasi ya Congo ni ya kutia wasi wasi. Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa wanajeshi na [...]

18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mamia ya wanawake na wasichana wadhulumiwa kimapenzi Goma

Kusikiliza / wasichana na wanawake, Goma

Karibu wanawake na wasichana 400 walibwakwa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati wa mapigano ya hivi majuzi kweneye mji wa Goma. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa huduma inatolewa kwa wanawake 278 na wasichana 117 waathiriwa wa dhuluma za kimapenzi. UNICEF inasema kuwa wanawake [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Haki za wahamiaji zilindwe: Jopo la wataalamu wa haki

Kusikiliza / siku ya wahamiaji

Jopo la wataalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, wataalamu wa haki za wahamiaji na Muungano wa nchi za bara la Amerika limeelezea wasiwasi wake kuhusu tabia ya baadhi ya nchi kuchukulia kitendo cha mtu kukosa nyaraka rasmi za ukaazi kama uhalifu. Katika taarifa ya pamoja kuadhimisha siku ya kimataifa [...]

18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zenye wahamiaji zitambue athari za majanga na mizozo kwa wahamiaji: IOM

Kusikiliza / wahamiaji

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji hii leo, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limetaka jumuiya ya kimataifa hususan nchi zinazotoa au kupokea wahamiaji kutambua athari za majanga na mizozo kwa wahamiaji. Msemaji wa IOM Jean Phillip Chauzy ametolea mfano wahamiaji Laki Mbili nchini Libya kutoka nchi maskini ambao mwaka 2011 walijikuta katika mazingira [...]

18/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031