Nyumbani » 17/12/2012 Entries posted on “Disemba 17th, 2012”

Ukarabati jengo la UM wachangia kupunguza uchafuzi wa mazingira: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amerejea katika ofisi yake iliyoko kwenye jengo kuu la umoja huo mjini New York, Marekani baada ya ukarabati uliodumu kwa takribani miaka mitano. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia katika ofisi yake hiyo, Bwana Ban amesema ukarabati huo ni wa kihistoria kwa kuwa umezingatia [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waasi wa M23 waripotiwa kukiuka azimio la UM: Waonekana Kivu Kaskazini

Kusikiliza / M23 Goma

Hali ya usalama katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini imeripotiwa kuwa ni ya wasiwasi baada ya waasi wa kikundi cha M23 kuonekana katika viunga vya mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martini Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo [...]

17/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Vita dhidi ya Malaria yakwamishwa na pesa: Tanzania Zanzibar, Rwanda na Zambia zang'ara katika kutokomeza Malaria

Kusikiliza / mbu

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2012 imeonyesha kupungua kwa ufadhili katika mipango ya vita dhidi ya ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu takribani Laki Sita na Elfu Sitini duniani kote. Idadi kubwa ya vifo hivyo ni vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Hata [...]

17/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Shambulio lingine nchini Iraq laua raia: Mjumbe wa Ban ataka pande husika zifanya mashaurino

Kusikiliza / Martin Kobler

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler, ameshutumu vikali msururu wa mashambulio ya jana na leo yaliyotokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 44 na wengine 77 wamejeruhiwa. Habari zinasema katika shambulio la leo alfajiri kaskazini mwa nchi hiyo lililolenga askari wa jeshi la Iraq na raia, watu [...]

17/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema anasikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria katika siku za karibuni na hatari kubwa inayokabili raia kwenye maeneo ambako kuna mapigano. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza masikitiko hayo huku akishutumu mashambulizi ya silaha kwenye maeneo ya raia ambapo amerejelea kauli yake ya kutaka pande [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vijana nchini Sudan Kusini kupokea mafunzo kuhusu amani na mapatano

Kusikiliza / Forest Whittaker

Huku asilimia 72 ya wakazi wa Sudan Kusini wakiwa chini ya umri wa miaka 30, Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO linaeleza kuwa ni bayana kwamba hatma ya taifa hilo iko mikononi mwa vijana. Ili kuweza kulea kizazi kipya balozi wa uhusinao mwema wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kujielisha kuhusu usalama wa nukilia wakamilika Japan

Kusikiliza / nembo ya IAEA

Naibu mkurugenzi mkuu kwenye masuala ya usalama wa nuklia kwenye Shirika la kudhibiti nishati ya atomic duniani IAEA Denis Floy amesema kuwa mkutano ambao umekamilika umetoa fursa nzuri wa kubadilishana ujuzi kutokana na ajali ya kituo cha Fukushima Daichi nchini Japan na pia kutoa mwelekeo wa kuwepo jitihada za kimataifa za kuhakikisha kuwepo usalama wa [...]

17/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNRWA yataka wakimbizi wa kipalestina wapatiwe ulinzi zaidi

Kusikiliza / wakimbizi, UNRWA

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu na kusimamia ulinzi kwa wakimbizi wa Kipalestina, lUNRWA Filippo Grandi ameiomba Syria na pande zote katika mzozo nchini humo kuhakikisha wakimbizi wa Syria, popote pale walipo nchini humo wanapatiwa ulinzi. Ombi la Grandi linafuatia picha zilizochapishwa na mashirika mbali mbali ya habari zinazoonyesha hali ya [...]

17/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNHCR kuanzisha kituo Jordan kuwafadhilia wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / raia wa Syria walio Jordan

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi António Guterres ametangaza kuanzishwa kwa kituo cha pamoja kitaratibu misaada ya kibinadamua kwa mamia ya wananchi wanaokimbia mapigano nchini Syria ambao hadi sasa wamefikia 250,000 waliopata hifadhi nchini Jordan. Kituo hicho ambacho kitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Jordan kinalenga kukabiliana na [...]

17/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Fedha zaidi zahitajika kudhibiti Malaria: WHO

Kusikiliza / nembo ya WHO

Shirika la afya duniani, WHO limesema dola Bilioni Tano zinahitajika kila mwaka kwa kipindi cha muongo mmoja ujao ili kuhakikisha tiba dhidi ya Malaria inapatikana duniani kote. Hata hivyo WHO imesema mpaka sasa ni nusu tu ya kiwango hicho ndicho kinapatikana na hivyo kukwamisha harakati za kupambana na ugonjwa huo. Dkt. Richard Cibulskis mtaalamu kutoka [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sudan yahitaji takribani dola Bilioni Moja kwa misaada ya kibinadamu mwaka 2012: OCHA

Kusikiliza / raia wa Sudan

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA limeeleza kuwa kati ya dola Bilioni Nane na Nusu zilizoombwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2013, takribani dola Bilioni Moja ni kwa ajili ya Sudan pekee. Sudan inahitaji fedha hizo kwa ajili ya miradi 364 ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kasi ya kukabili tatizo la Malaria imepungua: WHO

Kusikiliza / malaria

Shirika la Afya duniani WHO, limechapisha ripoti yake ya mwaka 2012 inayoaangazia tatizo la Malaria ambayo imesema kasi ya kukabiliana na tatizo hilo imekosa msukumo na kushuka kiasi. Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa katika mji Mkuu wa Liberia, Monrovia na rais wa taifa hilo, Ellen Johnson Sirleaf, imeonyesha kushuka kwa jitihada za kukabiliana na kasi ya ugonjwa [...]

17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031