Nyumbani » 14/12/2012
Entries posted on “Disemba 14th, 2012”
Kusikiliza /

Sauti yangu ina nafasi! Ni ujumbe wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoadhimishwa tarehe 10 Desemba mwaka huu, siku ambayo miaka 64 iliyopita lilipitishwa tamko la kimataifa la haki za kibinadamu. Mwaka huu ujumbe huo unatoa fursa kwa makundi yote hususan wanawake, vijana, makundi madogo, walemavu, wapenzi wa jinsia moja, mashoga na hata [...]
14/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN mjini New York, Marekani umemalizika kwa mataifa 12 kuitikia wito wa shirika hilo wa kuzitaka nchi dunia kuongeza juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Kupitia mpango mpya, COMMIT, nchi hizo ikiwemo Togo, Ufaransa, Marekani [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea zaidi ya dola 700,000 kufadhili shughuli za misaada kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha nchini Ufilipino, misaada ambayo ni pamoja na huduma za afya na malazi. Kulingana na ripoti IOM kwa ushirikiano na idara ya kijamii na maendeleo DSWD juma hili ilitoa msaada wa makao ya dharura kwa familia [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baada ya wiki mbili za majadiliano, huko Dubai, wajumbe wa mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU wamekubaliana kuhusu mkataba mpya wa mawasiliano ya simu. Taarifa ya ITU inasema madhumuni ya mkataba huo mpya ni kuwezesha muunganiko wa kirahisi zaidi wa dunia kwa kutumia teknolojia ya kisasa habari na mawasiliano, ICT. ITU [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wajumbe zaidi ya 160 waliokuwa wanakutana huko Doha, wamekamilisha hatua ya kwanza muhimu ya uandikaji wa rasimu ambayo inakusudia kutumika kwa ajili ya kuyafanyia marekebisho miongozo ya mawasiliano duniani. Kukamilika kwa rasimu hiyo kutafanikisha mageuzi ya sheria ambayo sasa itaruhusu uhuru wa kusafirisha taarifa duniani kote bila vikwazo vyovyote. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Jopo la wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi kuhusu mwelekeo wa rasimu ya katiba nchini Misri na kuitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha mwishowe Katiba inakuwa si ya kibaguzi bali inalinda usawa na kuendeleza haki za wanawake. Mmoja wa wataalamu hao Kamala Chandrakirana amesema mpaka sasa fursa muhimu ya [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kusikitishwa kwake na kutokuwepo kwa maendeleo ya dhahiri ya kurejesha utawala wa kikatiba nchini Guinea-Bissau. Katika taarifa yake, Baraza hilo imesema wajumbe wake 15 wanaamini kuwa utuliv unaweza kurejea kupitia mchakato utakaokubaliwa na pande zote kwa kuzingatia mashauriano ya dhati. Wajumbe hao wamerejelea azimio namba 2048 la [...]
14/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kikundi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kinacholinda amani huko Darfur, UNAMID kimekabidhi mahakama ya kijiji huko Tawilla, kaskazini mwa Darfur. Mahakama hiyo yenye lengo la kurahisisha utekelezaji wa shughuli za mahakama kwenye eneo hilo, ni sehemu ya miradi ya UNAMID ya kuleta mabadiliko yanayoonekana haraka, kwa lengo la kuleta amani [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kuwa watoto waliobakia bila makazi katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga huko Ufilipino wako hatarini kunyanyaswa na kutumikishwa. UNICEF inasema licha ya kwamba kazi nzuri imefanyika kukabiliana na madhara ya kimbunga, lakini mahitaji muhimu ya watoto hayatiliwi maanani na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kudhalilika ikiwemo kusafirishwa [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiwango cha malipo ya ujira nchini China kimeongezeka mara tatu kati ya mwaka 2000 na 2010 na hivyo kuonyesha dalili za uwezekano wa kuanza kutoweka kwa dhana iliyozoeleka ya ujira mdogo miongoni mwa wachina. Ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu malipo ya ujira imejumuisha viwango vya ujira katika mashiriak ya kiserikali na makampuni madogo [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea dola 700,000 pesa za Canada kufadhili shughuli za misaada kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha. Kulingana na ripoti IOM kwa ushirikiano na idara ya kijamii na maendeleo DSWD juma hili ilitoa msaada wa makao ya dharura kwa familia 600 au watu 30,000 ambao wamekuwa wakiishi nje tangu tufani hiyo [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mdororo wa kiuchumi duniani unazidi kuendelea kuathiri maendeleo ya nchi za Asia na Pasifiki ambapo taarifa hizo ni kwa mujibu wa makadirio mapya ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia-Pasifiki, ESCAP. Makadirio hayo yaliyotolewa leo huko Thailand yanaonyesha kuwa ukuaji uchumi katika nchi tajiri umeendelea kudorora [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takwimu za mwaka 2012 zilizochapishwa hii leo za shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuongezeka kwa mchango kutoka kwa nchi zinazoendelea kwa uchumi wa dunia kutokana hasa na uundaji wa meli na vifaa vya electroniki. Yakiongozwa na mataifa yaliyostawi ya Asia, mataifa yanayoendelea yameongeza mchango wao kwa mauzo ya nje ya [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umetangaza ombi la dola Bilioni 8.5 kwa ajili ya operesheni zake za misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2013. Fedha hizo zinalenga kuwahudumia watu Milioni 51 kutoka nchi 16 duniani ambao wanahitaji misaada ya kibinadamu. Katika usambazaji wa huduma hizo, jumla ya mashirika 520 ya misaada yatashirikiana na Umoja wa Mataifa kuwapatia misaada [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »