Nyumbani » 13/12/2012 Entries posted on “Disemba 13th, 2012”

Mapinduzi ya teknolojia ya simu yachochea maendeleo ya huduma za kijamii

Kusikiliza / Mwananchi akitumia simu kupata huduma za kijamii

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii duniain kote ikiwemo nchi zinazoendelea. Inaelezwa kuwa matumizi ya simu ikiwemo zile za mkononi ambazo kwa sasa zinaweza kutuma picha na hata sauti, zimeweza kuwa mkombozi kwa mwananchi wa kawaida. Mathalani wapo waliofungua vioski kwa ajili ya kutoa huduma za kutuma [...]

13/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Jeshi la Sudan Kusini lijizuie linapokabiliana na raia: UM

Kusikiliza / Walinda amani wa UNSMISS

  Umoja wa Mataifa umelitaka jeshi la Sudan Kusini kujizuia pindi linapokabiliana na raia. Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kimetoa taarifa hiyo kufuatia matukio ya hivi karibuni ya mapambano kati ya waandamanaji na polisi yaliyosababisha vifo vya raia Tisa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Taarifa hiyo imesema kwa sasa [...]

13/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ICC yatupilia mbali rufani ya rais wa zamani wa Ivory Coast

Baraza la Usalama

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC, wametupilia mbali madai yaliyotolewa na upande wa utetezi wa aliyekuwa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo waliodai kuwa majaji hao hawakustahili kuendesha kesi hiyo. Mawakili wanaomtetea Gbagbo waliwalisiha rufani kwenye mahakama hiyo wakidai kuwa majaji wanaoendesha kesi hiyo wanakosa nguvu za kisheria [...]

13/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Imani ndiyo nguzo kuu ya utoaji ulinzi wa jamii ya wakimbizi: UNHCR

Kusikiliza / nembo UNHCR

Zaidi ya watu 400 ikiwemo viongozi wa dini na wataalamu wa imani wamekusanyika mjini Geneva ambako wanajadiliana kuhusu tofauti za kiimani zinavyoweza kutoa mchango kuwasaidia watu wanaoandamwa na matatizo ikiwemo wakimbizi. Mkutano huo wa siku mbili unashabaha ya kuangalia kwa kiasi gani pamoja na kuwepo kwa tofauti za kidini, lakini bado imani hizo zikawa katika [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Taratibu za kuwafikisha watuhumiwa wa uhalifu Darfur zaendelea: Bensouda

Kusikiliza / Fatou Bensouda

Baraza la Usalama hii leo limepokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon kuhusu Sudan ambayo pamoja na mambo mengine imeelezea hatua zilizofikiwa katika kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa vitendo vya uhalifu huko Darfur. Ripoti hiyo imewasilishwa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, Fatou Bensouda ambaye [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano kati ya WFP na Saudi Arabia waokoa maisha ya mamilioni

Kusikiliza / Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin, amehitimisha ziara yake ya siku mbili huko Saudi Arabia na kusema kuwa ushirikiano kati ya pande mbili hizo umesaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kote. Katika mazungumzo yake na Mwanamfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud, Bi Cousin amesema [...]

13/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Idadi ya watalii kwa mwaka 2012 duniani kote leo yafikia Bilioni Moja

Kusikiliza / utalii

Idadi ya watalii waliotembelea dunia hii leo imetimia Bilioni Moja na kuweka rekodi mpya kwenye utalii wa kimataifa sekta inayochangia nafasi moja kwa kila ajira 12 duniani. Kwenye tarehe ya kuadhimisha mtalii nambari bilioni moja ambayo ni leo tarehe 13 shirika la utalii duniani UNWTO limetaja hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa na watalii kuhahakikisha kuwa safari [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Licha ya mafanikio safari bado ni ndefu kufikia usawa wa kijinsia: WU

Kusikiliza / Wu Hongbo

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya uchumi na kijamii, Wu Hongbo amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kufikia usawa wa kijinsia licha ya hatua zilizofikiwa kutokana na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia. Akizungumza katika mahojiano mjini Geneva, Uswisi, kabla ya mjadala kuhusu mbinu za kuimarisha usawa wa kijinsia na [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano njia pekee ya kulinda raia: UNAMID

Kusikiliza / Aïchatou Mindaoudou

Kaimu Mkuu wa kikundi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kinacholinda amani huko Darfur, UNAMID, Aïchatou Mindaoudou amesema ushirikiano miongoni mwa pande zote husika kwenye eneo hilo ndio njia pekee ya kuwezesha ulinzi wa raia. Bi. Mindaoudou amesema hayo baada ya ziara yake ya siku mbili katika maeneo ya Kusini na [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Umoja wa Mataifa laongeza muda wa kuhudumu kwa majaji kwenye mahakama ya ICTR

Kusikiliza / ICTR Rwanda

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu kwa majaji watano kwenye mahakama ya kimataifa inayosikiliza kesi za uhalifu wa kivita nchini Rwanda ICTR kwa lengo la kuiwezesha mahakama hiyo kumaliza kazi yake. Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania ilibuniwa baada ya kutokea mauaji ya halaiki nchini Rwanda ambapo [...]

13/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

ITU yaelezwa jinsi simu za mkononi zinavyoimarisha huduma za kijamii

Kusikiliza / simu ya mkono

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kusaidia kuimarisha sekta ya utoaji huduma mbali mbali nchini Tanzania, ikiwemo za afya na kiuchumi, na hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo Profesa John Nkoma ambaye yuko Dubai, Falme za kiarabu akishiriki mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU. [...]

13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930