Nyumbani » 12/12/2012 Entries posted on “Disemba 12th, 2012”

Baraza la Usalama lasikitishwa na kitendo cha DPRK: Kuchukua hatua iwapo itakiuka tena azimio

Kusikiliza / baraza la usalama

Wajumbe wa Baraza la Usalama leo wamefanya mashauriano kuhusu hofu na wasiwasi ulioibuka kufuatia kitendo cha Jumanne cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha roketi kwa kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu ambapo wameshutumu vikali kitendo hicho. Rais wa Baraza hilo Mohammed Loulichki amewaambia waandishi wa habari baada ya mashauriano hayo [...]

12/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usafirishaji haramu wa binadamu wakumba zaidi watoto: UM

Kusikiliza / watoto

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa vitendo vya usafirishaji watoto duniani vimeongezeka ambapo asilimia 27 ya waathirika wa vitendo vya usafirishaji wa binadamu duniani kote ni watoto. Ripoti hiyo ni matokeo ya utafiti uliofanywa kati ya mwaka 2007 na 2010 na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya [...]

12/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wanawake wanaoishi na virusi vya HIV wana nafasi kubwa ya kusaidia juhudi za dunia kukabiliana na kasi ya maambukizi mapya

Kusikiliza / WOMEN-OUT-LOUD

Ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI UNAIDS imesema kuwa dunia inaweza kupiga hatua kubwa kukabiliana na tatizo la kuenea kwa virusi vya ugon jwa huo iwapo wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi wakapewa nafasi ya kusikika. Ripoti hiiyo yenye kichwa cha habari kisemacho, sauti ya wanawake, imeorodhesha mafanukio [...]

12/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kamati ya UM juu ya haki za watoto yaalani kuendelea matukio ya kunyongwa watoto Yemen

Kusikiliza / kunyongwa kwa watoto nchini Yemen

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto Jean Zermatten, amelaani na vikali tukio la kunyongwa kwa mtoto mmoja wa kike Hind Al-Barti akisema kuwa kitendo hicho kilichotekelezwa mwezi huu mjini Sana'a nchini Yemen ni ukiukwaji mkubwa wa mikataba ya Umoja wa Mataifa. Duru zinasema kuwa mtoto huyo alikuwa na umri [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya demokrasia nchini Misri iko mashakani: IPU

Kusikiliza / IPU

Chama cha mabunge duniani, IPU kimesema harakati za kupigania demokrasia nchini Misri hazitakuwa na ukomo bila ya kuwepo kwa katiba inayokubaliwa na wananchi wote na ambayo pia itawahakikishia haki na usawa. Rais wa IPU Abdelwahad Radi amekaririwa akisema hayo huku akilaani matukio ya siku za karibuni ya ghasia na vifo nchini Misri na kitendo cha [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM yatoa nyongeza ya dola Milioni 23 kutokomeza Kipindupindu Haiti

Kusikiliza / kipindupindu, Haiti

Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa tishio nchini Haiti hali iliyolazimu Umoja wa Mataifa kutoa nyongeza ya dola Milioni 23 zaidi kusaidia vita dhidi ya ugonjwa huo. Nyongeza hiyo inajazia kiasi cha dola Milioni 118 ambazo Umoja wa Mataifa umeshatumia hadi sasa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo nchini Haiti. Nigel Fisher ni Naibu mwakilishi [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Unyanyasaji wa kijinsia bado ni tatizo kubwa Jamhuri ya Afrika ya Kati: Bangura

Kusikiliza / Hawa Zainab

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji wa kingono kwenye migogoro, Hawa Bangura amehitimisha wiki moja ya ziara yake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kueleza kuwa unyanyasaji wa kingono bado ni tatizo dhahiri nchini humo hasa maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vya kisiasa au kijeshi. Amesema kwa muda wote aliokuwepo [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa ayataka mataifa kulinda haki ya elimu hasa kwa msichana

Kusikiliza / mtoto msichana

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya elimu Kishore Singh ametoa wito kwa serikali kote duniani kuheshimu na kutekeleza wajibu wao wa kulinda haki ya elimu hasa kwa wasichana ambao wamepitia maisha magumu na walionyimwa elimu. Bwana Singh aliyasema alipohudhuria warsha moja mjini Paris yenye kauli mbiu "Mtetee malala au msichana, Elimu ni [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu alaani kitendo cha DPRK kukiuka azimio la UM

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani kitendo cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK cha kurusha roketi hapo jana kinyume na azimio la Umoja huo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amemkariri Bwana Ban akisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa kitendo hicho kimekiuka wito wa jumuiya ya kimataifa na azimio [...]

12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wafadhili waahidi dola milioni 384 kwa mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa mwaka 2013

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon na Valerie Amos

Wafadhili wamejitolea kuchanga jumla ya dola milioni 384 ambazo zitafadhili shughuli za dharura kuhudumia mamilioni ya watu wanaoathiriwa na majanga kufuatia ombi lililotolewa na Umoja wa Mataifa CERF. Akihutubia mkutano CERF uliondaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alimshukuru kila mmoja ambaye anajitolea kufadhili kuhakikisha [...]

12/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031