Nyumbani » 11/12/2012 Entries posted on “Disemba 11th, 2012”

Ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja au waliobadili jinsi ukome: Yvone Chaka Chaka

Kusikiliza / Yvonne Chaka Chaka

Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa  Yvonne Chaka Chaka  ambaye yuko mjini New York Marekani kushiriki tukio la ngazi ya juu la nafasi ya uongozi katika vita dhidi ya ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja au waliobadili jinsi zao amesema ni wakati muafaka serikali zinazobagua au kuhukumu watu hao zitajwe na ziabishwe kwa kuwa [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hofu ya usalama, mila na desturi zakwamisha matumizi ya vyoo

Kusikiliza / TOILETS

Umaskini pamoja na mila na desturi ni baadhi ya mambo yanayosababisha usafi duni miongoni mwa nchi maskini. Usafi huu duni unamulika zaidi matumizi ya vyoo salama ambapo inaelezwa kuwa kutokana na baadhi ya mila baadhi ya watu wanalazimika kujisaidia haja kubwa vichakani na hivyo kuhatarisha kuenea kwa magojwa kama vile kipindupindu. Shirika la afya duniani, [...]

11/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mjadala wa kitaifa ufanyike haraka Mali ili kuepusha mizozo: Ban

Kusikiliza / Cheick Modibo Diarra

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anakwazika na mazingira yaliyosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Mali, Cheick Modibo Diarra huku akitaka jeshi liache kuingilia masuala ya kisiasa na uongozi wa Mali umalize mivutano yote kwa njia ya amani.Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza kuwa matukio ya hivi karibuni huko Mali yanaonyesha [...]

11/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tumejizatiti kuridhia jeshi kwenda Mali: Baraza Kuu la UM

Kusikiliza / Baraza Kuu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani kitendo cha jeshi nchini Mali kumkamata Waziri Mkuu wa nchi hiyo Cheik Modibo Diarra na kusababisha kujiuzulu kwa serikali. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho ni kinyume na maazimio ya Baraza hilo yanayolitaka jeshi hilo lisiingilie kazi ya mamlaka za mpito nchini Mali. Kwa kauli moja [...]

11/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Milima yazidi kuporwa, maisha ya wakazi wake yazidi kuwa duni

Kusikiliza / Mlima Kilimanjaro

Milima ni tegemeo la wakazi wa dunia kwa shughuli na huduma mbali mbali ikiwemo maji ya kunywa, umwagiliaji, shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii na kadhalika. Hata hivyo maendeleo ya binadamu yamekuwa kikwazo kwa milima kuweza kutoa huduma hizo na hata kuhatarisha maisha ya wakazi au jamii za milimani. Katika siku ya kimataifa ya milima duniani [...]

11/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira zaidi ya wanaume: ILO

Kusikiliza / wanawake na ajira

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira kwa viwango vikubwa zaidi ya wanaume kote duniani, huku matarajio ya hali hiyo kurekebishwa yakiwa adimu katika miaka ijayo, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Ajira Duniani, ILO. Ripoti hiyo ya ILO kuhusu mienendo ya kimataifa kuhusu wanawake mwaka 2012, inaangalia mapengo yaliyopo ya kijinsia katika nafasi za [...]

11/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya shule 600 ziliibiwa vifaa au kuharibiwa huko DRC: UNICEF

Kusikiliza / MONUSCO DRC

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema shule 250 zilizokuwa zinatumika kuhifadhi wakimbizi wakati wa mzozo huko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC zimepora vifaa au zimeharibiwa na hivyo kufanya idadi ya shule zilizoathirika na mzozo huo kufikia 600. Ripoti ya UNICEF inasema kuwa takribani wanafunzi 240,000 wameshindwa kwenda shule [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa yazungumzia kuuawa kwa wanafunzi kwenye chuo kimoja mjini Khartoum

Kusikiliza / maandamano ya wanafunzi nchini Sudan

Ofiki ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa hivi majuzi kati ya wanafuzni na polisi mjini Khartoum nchini Sudan. Habari zinasema wanafunzi waliandamana kwa siku tatu mfululizo wakilalamikia vifo vya wanafunzi wannne wa chuo cha El- Gezira kilicho kati kati mwa Sudan. Hii ni baada ya [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WHO kizindua ripoti kuhusu ugonjwa wa Malaria Jumatatu hii

Kusikiliza / mbu wa kuambukiza  Malaria

Shirika afya duniani WHO Jumatatu hii linatarajiwa kuzindua ripoti kuhusu ugonjwa wa Malaria duniani. Ripoti hiyo inaangazia jitihada zinazondelea za kupambana na ugonjwa wa Malaria na athari za kupungua kwa ufadhili kwenye vita dhidi ya ugonjwa huo. Ripoti hiyo pia inaonyesha hatua zilizopigwa katika kutimizwa kwa lengo la kupunguza ugonjwa wa Malaria kote dunaini kwa [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya wasyria nusu milioni sasa ni wakimbizi kwenye nchi majirani: UNHCR

Kusikiliza / msaada nchini Syria

Idadi ya raia wa Syria waliokimbia na kuingia nchi majirani kwa sasa imepita watu nusu milioni kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. UNHCR inasema kuwa karibu wasyria 510,000 wamesajiliwa au wanaendelea kusajiliwa nchini Lebanon, Iraq, Uturuki na Kaskazini mwa Afrika. UNHCR inasema kuwa chini ya nusu ya wakimbizi waliosajiliwa [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Maisha duni ya wakazi wa milimani, hatua kuchukuliwa kuboresha maisha yao

Kusikiliza / siku ya milima duniani

Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Richard Muyungi amesema hali ya milima na maisha ya wakazi wake iko hatarini zaidi hivi sasa kutokana na shughuli za binadamu zinazosababisha mabadiliko ya tabia nchi. Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahamiaji wa Ethiopia waliokuwa wamekwama Yemen warejeshwa makwao: IOM

Kusikiliza / wakimbizi wa Ethiopia

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewarejesha makwao kwa ndege raia 210 wa Ethiopia waliokuwa wamekwama huko Yemen baada ya kushindwa kuingia Saudi Arabia kutafuta ajira. IOM inasema imegharimu dola Milioni Mbili nukta Moja ambazo ni msaada kutoka Uholanzi kusafirisha raia hao ambao wanafikisha idadi ya raia 9,500 wa Ethiopia waliorejeshwa nyumbani kutoka Yemen kwa [...]

11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031