Nyumbani » 10/12/2012 Entries posted on “Disemba 10th, 2012”

Dola milioni 65 zahitajika kusaidia Ufilipino baada ya Kimbunga Bopha

Kusikiliza / Madhara yaliosababishwa na Kimbunga Bopha

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kibinadamu leo wametoa ombi la dola milioni 65 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kusaidia mamilioni ya watu walioathirika kutokana na Kimbunga Bopha huko Ufilipino. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), fedha zitatumika katika Mpango unaojulikana kama Action Recovery Plan [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Baraza Kuu la UM laadhimisha miaka 30 ya mkataba kuhusu sheria ya bahari

Kusikiliza / law of the sea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon ametaka kuongezwa kwa shime zaidi duniani ili nchi zote zitie saini na kuridhia mktaba wa kimataifa wa sheria ya bahari, ambao mara nyingi hutambuliwa kama Katiba ya masuala ya bahari. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa mkataba [...]

10/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ushirikiano wa UNIFIL na LFA umeleta utulivu Kusini mwa Lebanon: Eliasson

Kusikiliza / Jan Eliasson

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson aliyeko ziarani nchini Lebanon ametembelea kikosi cha muda cha kulinda amani nchini humoUNIFIL na kusema kuwa ushirikiano kati ya kikosi hicho na majeshi ya Lebanon, LAF umeleta amani ya aina yake Kusini mwa Lebanon. Bwana Eliasson ametoa kauli hiyo baada ya kupatiwa maelezo ya operesheni za [...]

10/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakiukaji wa haki wawajibishwe: Maafisa UM

Kusikiliza / Rashid Manjoo

Katika kilele cha kampeni ya siku 16 ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia inayoenda sambamba na siku ya haki za binadamu hii leo, maafisa wa Umoja wa Mataifa wametaja ujumbe unaozingatiwa wakati huu ambao ni pamoja ukweli, haki na uwajibishwaji wa wale wanaokiuka haki hizo. Maeneo yaliyokumbwa na machafuko ya vita ndiyo yanayolengwa [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yaratibu kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia

Kusikiliza / uanaharakati dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia, UNAMID

Huko Darfur, Sudan, siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zimefikia kilele leo ambayo ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu, ambapo kampeni ya kupinga vitendo hivyo iliratibiwa na kikundi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika cha kulinda amani kwenye eneo hilo, UNAMID. Kampeni ilianza tarehe 25 mwezi [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNESCO yafanya hafla ya kumuunga Malala mkono

Kusikiliza / unescomalala

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, leo limefanya hafla ya kumuunga mkono msichana wa Kipakistani, Yousufzai Malala, na elimu ya mtoto wa kike. Hafla hiyo ambayo imeandaliwa na UNESCO pamoja na serikali ya Pakistan, imefanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa, sambamba na siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Dhamira ya [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya tahadhari huko Sahel inazidi kujitokeza: Ban

Kusikiliza / watoto, Sahel

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema hali ya tahadhari inazidi kujidhirisha kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika na hivyo ni muhimu hatua za haraka zikachukuliwa kukabiliana na hali hiyo. Bwana Ban ametoa kauli hiyo leo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ambalo limekuwa na mjadala [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umiliki wa simu za mkononi umepanda katika nchi nyingi zaidi: ITU

Kusikiliza / Simu za mkononi

  Takwimu za hivi karibuni za shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU, kuhusu hali ya teknolojia duniani zinaonyesha kuwa mwanzoni mwa mwaka 2012, kulikuwa na nchi saba ambako umiliki wa simu za mkononi ulizidi asilimia 200, ikimaanisha kuwa kila mtu alikuwa na zaidi ya simu mbili. Uchina ndiyo nchi ya kwanza duniani kuwa na watu [...]

10/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka wanawake na makundi madogo yapewe nafasi katika kutoa maamuzi

Kusikiliza / Navi Pillay

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ameshutumu kuendelea kutengwa kwa wanawake na makundi mengine madogo kukosa kushirikishwa kwenye masuala ya umma moja kwa moja au kupitia waakilishi wao. Pillay amesema kuwa kuwatenga wanawake hakuwanyimi tu haki zao za binadamu lakini pia fursa ya kujenga maisha yao ya baadaye. Akiongea mjini [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi mkuu wa ILO aelezea wasi wasi wake kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Tunisia

Kusikiliza / Guy Rider

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder ameelezea wasi wasi wake kutokana na matukio ya hivi majuzi ambayo yameshuhudiwa nchini Tunisia hasa ghasia zinazoendeshwa dhidi ya viongozi wa vyama vya wafanyikazi na ofisi za chama cha wafanyikazi nchini Tunisia (UGTT). Bwana Ryder amesisitiza kuwa mashirika ya wafanyikazi na yale ya waajiri hayawezi [...]

10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031