Nyumbani » 06/12/2012 Entries posted on “Disemba 6th, 2012”

Kimbunga Bopha chasababisha vifo na uharibifu wa mali Ufilipino; Ban atuma salamu za pole

Kusikiliza / kimbunga

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya watu, majeruhi na uharibifu wa mali na miundombinu kutokana na kimbunga Bopha au Pablo kilichokumba eneo la Mindanao huko Ufilipino. Katika taarifa yake Bwana Ban ametuma salamu za pole kwa serikali ya Ufilipino na familia zilizopoteza jamaa au kujeruhiwa kutokana na [...]

06/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano kuhusu chanjo ya watoto wafanyika Tanzania

Kusikiliza / chanjo ya watoto

Wataalamun wa afya pamoja na watunga sera kutoka mataifa mbalimbali duniani pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wameanzisha mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kujadilia hali ya utoaji chanjo na namna ya kukabiliana na magonjwa yanayoweza kutibika kwa watoto. Mkutano huo ambao umewajumuisha wajumbe zaidi ya 600, umehusisha Shirika la idadi ya watu UNFPA [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Awamu ya pili ya kampeni ya chanjo ya Homa ya Manjano kuanza mwezi huu Darfur

Kusikiliza / homa ya manjano, Darfur

Awamu ya pili ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano huko Darfur nchini Sudan inatarajiwa kuanza mwezi huu ili kudhibiti ugonjwa huo uliolipuka mwezi Septemba mwaka huu ambapo watu 165 wameshakufa kutokana na ugonjwa huo huku 732 wakishukiwa kuugua kwenye vitongoji 33 kati ya 64 vya jimbo la Darfur. Wizara ya afya ya [...]

06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mpango mpya wa kuwasaidia wanawake kwenye vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa wazinduliwa

Kusikiliza / mabadiliko ya hali ya hewa

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kwa ushirikiano na wakfu wa Rockefeller hii leo wamezindua mpango mpya ya kutambua wajibu wa wanawake kwenye vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mpango huo una lengo la kuonyesha mambo yanayozishauri serikali, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhusu wajibu wa [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rais Assad wa Syria akabiliwe na sheria iwapo atatumia silaha za kemikali: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kwamba rais wa Syria Bashar al-Assad atawajibika kisheria iwapo serikali yake itatumia silaha za kemikali kukabiliana na upinzani nchini Syria. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad, Iraq, ambako amekutana pia na Waziri Mkuu, Nuri al-Maliki. Bwana Ban amesema ameelezea [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mtandao wa intaneti wakatika kwenye mkutano wa kimataifa wa mawasiliano

Kusikiliza / ITU

Mawasiliano ya mtandao na moja ya tovuti za shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU yalikatika kwa saa mbili na kusababisha mkanganyiko mkubwa miongoni mwa washiriki na wafuatiliaji wa mkutano wa kimataifa wa mawasiliano huko Dubai. Kukatika kwa mawasiliano ya intaneti kulisababisha washiriki na wafuatiliaji kushindwa kupata nyaraka muhimu kutoka kwenye mtandao kwa kuwa mkutano huo [...]

06/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya kulinda na kusaidia wanaohama yaanza kutekelezwa

Kusikiliza / wakimbizi wa Congo

Makubalano ya Muungano wa Afrika kuhusu usalama na misaada kwa wakimbizi wa ndani yanayojulikana pia kama makubaliano ya Kampala yameanza kutekelezwa hii leo baada ya jumla ya mataifa 15 kuyaunga mkono. Makubaliano hayo yanatoa mpangilio wa kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi wa ndani na kuyataka mataifa ya Afrika kuzuia uhamiaji . Kamishna mkuu wa Shirika la [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

FAO yataka mataifa kuelekeza asilimia kubwa ya uwekezaji kwenye kilimo

Kusikiliza / FAO

Uwekezaji ulio bora kwenye kilimo ni moja ya njia madhubuti za kuangamiza njaa na na umaskini na pia kulinda mazingira. Hii ni kwa mujibu wa ripoti yenye kichwa "Hali ya chakula na kilimo mwaka 2012" iliyotolewa hii leo mjini Rome. Ripoti hiyo inasema kuwa wakulima zaidi ya bilioni moja duniani wanastahili kupewa kipaumbele katika uwekezaji [...]

06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hakuna mtu anayestahili kutengwa katika kufurahia haki zake: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

Wakati zimesalia siku chache tu kabla ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema hakuna mtu hata mmoja anayestahili kutengwa katika kufurahia haki zake, kama zilivyowekwa katika azimio la kimataifa la haki za binadamu. Bi Pillay amesema kuwa mamilioni ya watu ambao [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bei ya chakula iliendelea kushuka mwezi Novemba: FAO

Kusikiliza / bei ya vyakula

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema wastani wa bei ya chakula umeendelea kushuka ambapo kwa mwezi uliopita wa Novemba ulishuka kwa asilimia Moja nukta Tano, ikilinganishwa na mwezi uliotangulia. Ripoti ya FAO kuhusu bei za chakula inaonyesha kuwa bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi Tatu na kufikia pointi [...]

06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi wa kipalestina waomba UNRWA isisitishe operesheni zake huko Syria

Kusikiliza / Filipo Grandi

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada na usalama kwa wapalestina, UNRWA, Filippo Grandi amekagua operesheni za shirika hilo huko Yarmouk, Syria ambako wafanyakazi 3,700 wanaendelea kutoa huduma za kijamii licha ya mzozo unaoendelea. Huduma hizo ikiwemo elimu na afya ni kwa ajili ya zaidi ya wakimbizi 500,000 wa kipalestina ambapo [...]

06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031