Nyumbani » 05/12/2012 Entries posted on “Disemba 5th, 2012”

Kuwait na Iraq zina fursa nzuri zaidi za kuimarisha uhusiano wao: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyeko ziarani Mashariki ya Kati, hii leo alitembelea Kuwait ambako ameeleza kutiwa moyo na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi na Iraq, uhusiano ambao amesema unazidi kuimarika. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mkuu wa Kuwait, Kuwait City, Bwana Ban amesema anaamini kuwa nchi mbili hizo [...]

05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yalaani shambulio la jana dhidi ya shule huko Damascus

Kusikiliza / Damascus

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limelaani shambulio la jana kwenye shule moja iliyoko karibu na mji mkuu wa Syria Damascus ambalo lilisababisha mauaji ya wanafunzi kadhaa pamoja na mwalimu mmoja. Mkurugenzi wa UNICEF kwa Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Maria Calivis amesema katika taarifa yake kuwa tangu kuanza [...]

05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uwanja wa ndege wa Goma waanza tena kutoa huduma: UM

arik-air_1

Umoja wa Mataifa umesema Uwanja wa ndege wa Goma, Mashariki wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, umefunguliwa leo na unatoa huduma baada ya kufungwa kufuatia waasi wa kikundi cha M23 kuingia na kusonga ndani ya mji huo mwezi uliopita. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya usalama huko Mali bado si nzuri: Ban

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Baraza la Usalama leo limepatiwa taarifa ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu hali ya usalama ilivyo huko Mali Afrika Magharibi ambapo amesema hali ya usalama si nzuri na anaunga mkono mapendekezo ya Afrika kuhusu ulinzi na usalama nchini Mali. Ripoti hiyo imewasilishwa na Msaidizi wa Bwana Ban kwa masuala ya [...]

05/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Israel yatakiwa kuheshimu makubaliano yaliyomaliza mapigano Gaza

Kusikiliza / Richard Falk

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kwenye maene ya kipalestina yanayokaliwa na Israel tangu mwaka 1967 Richard Falk ametoa wito kwa Israel akiitaka itekeleze makubaliano yaliyositisha mzozo kwenye ukanda wa Gaza. Falk aliyasema hayo alipofanya ziara kwenye ukanda wa Gaza na Misri ambapo alikutana na waakilishi wa mashirika [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhaba wa Maji Darfur wapatiwa suluhisho: UNAMID

Kusikiliza / UNAMID

Tatizo la uhaba wa maji katika jimbo la Darfur huko Sudan limepatiwa ufumbuzi baada ya kikundi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni humo, UNAMID na benki ya Maendeleo ya Afrika, kwa ushirikiano na serikali ya Sudan kuzindua miradi kadhaa ya maji kwenye eneo hilo. Miradi hiyo yenye lengo la kukidhi [...]

05/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Watu zaidi bado wanahitaji msaada ukanda wa Gaza: OCHA

Kusikiliza / wakimbizi wa Gaza

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas chini ya uongozi wa Misri yaliyoanza kutekelezwa tarehe 21 mwezi Novemba yamewafanya wapalestina wengi kuyafikia maeneo ya uvuvi na kilimo ambayo awali hawakuwa wakiyafikia. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa kulingana na ya tathmini iliyoendeshwa ni kwamba [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu hujitolea stadi na uwezo wao kusaidia wengine: UNV

Kusikiliza / uwezo wa kusaidia

Mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa, UNV umesema kila mwaka mamilioni ya watu duniani kote hujitolea muda wao na stadi zao kubadili maisha ya watu wengine. UNV imesema hayo leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kujitolea ambapo msemaji wake Jennifer Stapper amesema ni fursa ya kutoa shukrani kwa wafanyakazi wa kujitolea wanaotekeleza majukumu [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kupima viwango vya risasi mchangani kutapunguza madhara kwa watoto

Kusikiliza / risasi mchangani

Nchi nyingi, hususani zile zenye historia ndefu ya uchimbaji migodi zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara ya madini ya risasi miongoni mwa watoto kwa kupima viwango vya uchafuzi wa madini hayo mchangani, ili kutambua ni maeneo yepi yenye hatari, na hivyo kuwaepusha watoto na maeneo hayo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ilochapishwa [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nokia yapiga jeki mpango wa UNFPA kuhusu uzazi salama

Kusikiliza / UNFPA

Kampuni ya simu ya Nokia imetangaza kuunga mkono jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA na kwa kuanzia kampuni hiyo ya simu imekubali kuchangia kiasi vifaa vya kujifungulia vipatavyo 3,000 ambayo yanakusudia kufanikisha uzazi salama. Uchangiaji wa huduma hiyo ni sehemu ya uungwaji mkono wa kampeni iliyoanzishwa [...]

05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kazi ya kujitolea imesaidia kutekeleza Malengo ya Milenia: Ban

Kusikiliza / Siku ya Kimataifa ya kujitolea

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kujitolea hii leo na kusema kuwa kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kujitolea inasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia ya mwaka 2015. Katika ujumbe wake Bwana Ban amesema wafanyakazi hao wakiwemo 7,700 wa Umoja wa Mataifa wameshiriki kazi mbali [...]

05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031