Nyumbani » 03/12/2012 Entries posted on “Disemba 3rd, 2012”

Hali mbaya ya usalama Syria: UM kusitisha baadhi ya shughuli zake

Kusikiliza / Martin Nesirky

Umoja wa Mataifa umesema unasitisha baadhi ya shughuli zake nchini Syria pamoja na kuondoa watendaji wake ambao si lazima wawepo nchini humo kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama. Msemaji wa umoja huo Martin Nesirky amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo akikariri Idara ya Usalama [...]

03/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Pande zinazozozana Yemen zaahidi kutoandikisha watoto jeshini: Zerrougui

Kusikiliza / Leila Zerrougui

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya watoto na mizozo ya kivita, Leila Zerrougui amesema pande zinazozona nchini Yemen zimekubaliana kuachana na mpango wa kuandikisha watoto kwenye majeshi yao. Kauli hiyo ya Zerrougui ameitoa leo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, [...]

03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNESCO yazindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi walemavu kutumia teknolojia ya mawasiliano

Kusikiliza / six-languages

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limezindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kupata fursa ya kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari, ICT. Ripoti hiyo imetolewa hii leo ambayo ni siku ya watu wenye ulemavu duniani na imechapishwa katika lugha Sita, ambazo ni kiingereza, kifaransa, kispaniola, kichina, kiarabu, kirusi na [...]

03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Matumaini ya kuimarika sekta ya viwanda duniani, yayoyoma: UM

Kusikiliza / viwanda

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imebainisha kuyoyoma kwa matumaini ya kukua kwa sekta ya viwanda duniani. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO limetoa takwimu za sekta ya viwanda kwa robo ya tatu ya mwaka huu ambazo zinaonyesha kuwa kiwango cha ukuaji kwenye sekta hiyo kilikuwa asilimia 2.2 ikilinganishwa [...]

03/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kutathmini mkataba wa Ottawa waanza Geneva

Kusikiliza / landmine.jpg

Mkutano wa mwaka wa nchi wa wanachama wa Mkataba wa kuzuia mabomu ya kutegwa ardhini yanayolengwa binadamu umeanza huko Geneva Uswisi ambapo wawakilishi wa serikali, taasisi za kiraia pamoja na wataalamu wanajadili kwa wiki nzima na kufanyia tathmini mkataba huo ujulikanao kama Ottawa Convention. Rais wa mkutano huo Balozi Matjaz Kovacic kutoka Slovenia amesema mkutano [...]

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAMID yasaidia harakati za kupambana na homa ya manjano Darfur

Kusikiliza / Homa ya Manjano, Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa usaidizi huko Darfur, UNAMID umetia shime katika juhudi za kupambana na homa ya manjano kwenye jimbo hilo ambapo imesaidia usafirishaji wa vifaa kwenda maeneo ambako kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo inatekelezwa. Kaimu Mkuu wa UNAMID Aïchatou Mindaoudou amesema ofisi yake inajisikia [...]

03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mikakati ya Bangladesh ya kujiandaa dhidi ya majanga ni mfano wa kuigwa: UM

Kusikiliza / majanga, Bangladesh

Mratibu Mkuu wa Masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametembelea Bangladesh kujionea jinsi nchi hiyo inavyojiandaa dhidi ya majanga ambapo amesema mikakati ya nchi hiyo ni mfano wa kuigwa. Bi. Amos ametaja mikakati hiyo ni pamoja na nchi hiyo kuwekeza mbinu za kujiandaa dhidi ya majanga kwa wananchi wenyewe kutokana na nchi [...]

03/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wananchi wa kawaida ndio wanaondelea kutaabika zaidi nchini Syria

Kusikiliza / wakimbizi wa Syria

Wakati hali inapoendelea kuwa mbaya nchini  Syria kila siku wale wanaoiahama na waliosalia wote wanazidi kukumbwacha changamoto nyingi. Kuendelea kuwepo ukosefu wa usalama kumewapa wakati mgumu wahudumu wa kibinadamu wanaotoa misaada kwa watu walioathiriwa. Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Syria Radhouane Nouicer anasema kuwa wanajaribu kutafuta njia za kuwafikia watu zaidi wanaohitaji misaada kulingana [...]

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Katibu Mkuu Ban Ki-moon: WCIT 2012

03/12/2012 | Jamii: Mawasiliano mbalimbali | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono Intaneti huria: Ban

Kusikiliza / technology

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono uhuru wa kujieleza kupitia mtando wa intaneti, akiongeza kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inazidi kubadilisha ulimwengu kwa kuwafungulia watu milango ya ufanisi, kuokoa maisha, kutoa elimu na kuwapa uwezo zaidi. Akitaja mfano wa mabadiliko ya kisiasa katika nchi [...]

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Israel isitishe mpango wa ujenzi wa makazi mapya Jerusalem Mashariki: Ban

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Mpango wa Israel wa kujenga makazi mapya Elfu Tatu huko Jerusalem Mashariki na sehemu zingine za Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan umeripotiwa kumsikitisha na kumkatisha tamaa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, na hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wake. Taarifa zaidi na Monica Morara. (SAUTI YA MONICA MORARA)  

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuwalinda raia ni jambo la kipaumbele wakati M23 wanaondoka Goma: OCHA

Kusikiliza / M23, Goma

Siku kumi na mbili baada ya waasi wa M23 kuutwaa mji wa Goma, hali ya kibinadamu na ya kiusalama bado inatia wasiwasi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Takriban watu 130, 000 wamelazimika kuhama makwao na wanaishi katika kambi na makazi mengine ya dharura karibu na, au katika mji wa [...]

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jitihada za kuwapatia walemavu haki zao ziimarishwe: Ban

Kusikiliza / siku ya walemavu duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza ahadi nzuri zinazotolewa kwa ajili ya kuimarisha maisha ya zaidi ya watu bilioni Moja wanaoishi na ulemavu duniani kote. Ban katika ujumbe wake wa siku ya walemavu duniani hii leo, amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa changamoto kubwa hivi sasa ni [...]

03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930