Nyumbani » 30/12/2012
Entries posted on “Disemba, 2012”
Kusikiliza /

Kambi ya Dadaab iliyoko Kaskazini Mashariki mwa Kenya inahifadhi wakimbizi kutoka Somalia. Kambi hii inaelezwa kuwa ni kubwa kuliko kambi zote za wakimbizi duniani ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya Laki Nne na Nusu. Uhaba wa maji umekuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo. Lakini nuru imechomoza na kubadili maisha ya familia za kifugaji. Ni nuru gani hiyo? [...]
30/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Hatimaye mwaka 2012 umefikia ukingoni. Kwa Umoja wa Mataifa Katibu Mkuu, Ban Ki Moon alieleza kuwa ulikuwa wa mtikisiko, kuanzia mabadiliko ya tabia nchi, mapigano nchini Syria na mzozo Mashariki ya Kati, mgogoro Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, mapigano huko Mali, majanga ya asili ikiwemo vimbunga, mafuriko, njaa yote alisema yaliuweka Umoja wa Mataifa [...]
30/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa nchi za kiarabu katika mzozo wa Syria, Lakhdar Brahimi Jumamosi atakuwa na mazungumzo na Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi, Sergei Lavrov, mjini Mosciw, ikiwa ni katika jitihada za kupatia suluhu mgogoro wa Syria. Taarifa hizo ni kwa mujib uwa msemaji wa Umoja wa [...]
28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, MONUSCO umesema helikopta zake mbili zilishambuliwa Jumatano usiku kaskazini mwa mji wa Goma. Taarifa ya MONUSCO inaeleza kuwa helikopta hizo zilikuwa katika safari zake za kawaida za kuthibitisha ubora wake wa kuruka ambapo moja ilishambuliwa huko Kibumba na nyingine Kanyamahoro, [...]
28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Makala yetu wiki hii ambayo pia ni ya mwisho kwa mwaka huu wa 2012 inaangazia Azimio la aina yake lililopitishwa na Umoja wa Mataifa la kupiga vita ukeketaji wa wanawake. Harakati za kupiga vita ukeketaji wa wanawake, wasichana na watoto wa kike zinazidi kuzaa matunda. Na hatua ya hivi karibuni zaidi ni ile ya Baraza [...]
28/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Taifa la Sudan Kusini lililopata uhuru wake mwaka 2011 limejumuishwa rasmi katika orodha ya nchi maskini duniani na kufanya idadi ya nchi hizo kufikia 49. Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendeleo UNCTAD, limesema Sudan Kusini imejumuishwa tarehe 18 mwezi huu na hivyo ina haki ya kupata misamaha kadhaa ili iweze kuondokana na [...]
28/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP limesema halimtambui Artur Baptista da Silva, mtu ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa ni msemaji wake wa masuala ya Uchumi kwa Ureno na Ulaya Kusini. Taarifa ya UNDP imesema Da Silva siyo mtumishi wala hajawahi kuajiriwa na shirika hilo na kwamba maoni yoyote aliyotoa ni ya kwake [...]
28/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maelfu ya wananchi wa Pakistan ambao waliathiriwa na mafuriko ya mwezi wa Septemba bado hawajarejea kwenye maeneo yao ya awali. Mashirika ya kutoa misaada yamesema kuwa idadi kubwa waathirika hao bado wanaendelea kusalia kwenye makambi na wengine kwenye mabanda kufuatia maeneo yao kuharibiwa vibaya na mafuriko. Kiasi cha watu milioni 4.8 wanaripotiwa kuathiriwa na mafuriko [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Teknolojia mpya na ya kisasa ndiyo iliyotajwa kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuyafikia mahitaji ya wakimbizi wengi wa Sudan Kusin. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, linatumia teknolojia mbalimbali ikiwemo mifumo ya satelite pamoja na mifumo mengine ya kiteknolojia kuwafikishia ujumbe wakimbizi hao. Pia shirika hilo linatumia teknolojia hiyo kutoa misaada ya [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limekamilisha oparesheni ya siku nne ya kuwagawia misaada isiyo chakula watu 6,500 waliohama makwao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. Kati ya misaada iliyosambazwa kwenye eneo la Bulengo ni pamoja na matandiko ya kulalia, mablanketi, sabuni, vyombo vya jikoni na pia nguo. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (SAUTI [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la afya duniani WHO limefanya tathmini ya kazi yake mwaka 2012 hasa jitihada za kukabiliana na magonjwa likisema kuwa mengi yalitimizwa mwaka huu ikiwemo kukomesha kusambaa kwa ugonjwa wa kupooza nchini India na kutimizwa kwa lengo la maendeleo ya Milenia la maji ya kunywa kabla ya muda wa mwisho. Taarifa kamili na Monica Morara. [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kliniki ya muda iliyoanzishwa kwenye kambi ya Mugunga mjini Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC kwa ajili ya kusaidia wanawake waliokumbwa na visa vya ubakaji imeripotiwa kuwa mkombozi kwa makumi ya wanawake na wasichana waliokumbwa na mkasa huo. Afisa wa tiba katika kituo hicho Barubeta Maombi amesema msaada wanaotoa ni wa vipimo [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake juu ya hali ya Usalama huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kushutumu vikali mashambulizi yanayoendelea kufanywa na kikundi cha waasi kiitwacho SELEKA kwenye miji mbali mbali nchini humo. Taarifa ya Baraza hilo imekariri wajumbe wake wakisema kuwa kitendo hicho kinakwamisha makubaliano ya amani ya [...]
28/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwezi Disemba mwaka 2012 Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha azimio kuhusuu shirika lake linalohusika na mazingira, UNEP. Je azimio hilo lina malengo yapi na manufaa yake ni nini? Tujiunge na Monica Morara. “We now take a decision on draft resolution entitled, Report of the Governing Council of the United Nations Environment Programme …. [...]
27/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Msuluhishi wa Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya kiarabu kwa mzozo wa Syria Lakhdar Brahimi amependekeza serikali mpito nchini humo itayokuwa kwenye hatamu za uongozi hadi wakati kipindi cha utawala wa rais Bashar Al Assad kitapomalizika mwaka 2014. Kauli hiyo ambayo imenukuliwa na vyombo vya habari, inafuatia majadiliano ya kina yaliyofanywa baina ya Brahim na [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeitaka serikali ya Urusi kuzingatia maslahi ya watoto katika mapendekezo yake mapya ya kupiga marufuku raia wa Marekani kuasili watoto wa kirusi. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Anthony Lake katika taarifa yake amesema mapendekezo yaliyopitishwa na bunge la Urusi la kuweka marufuku [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM limeanza kutoa msaada kwa waathirika wa mvua kubwa, upepo mkali na maporomoko ya udongo yaliyokumba Sri Lanka wakati wa msimu huu wa sikukuu. Habari zinasema watu zaidi ya Laki Tatu kwenye wilaya 20 nchini humo wameathirika na hali hiyo ambapo eneo lililoathirika zaidi ni wilaya ya Batticoloa, [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani vikali mashambulzi yaliyoendeshwa kwenye miji kadhaa nchini Jamhuri ya Afrika ya kati na kundi la waasi la SELEKA. Ban amesema kuwa vitendo kama hivyo huwa vinahujumu makubaliano na jitihada za jamii ya kimataifa za kuleta amani chini humo. Amesema kuwa Umoja wa Mataifa uko tayari kulisaidia [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF wa kutoa msaada kidogo wa fedha kwa jamii maskini katika nchi zinazoendelea ili kujikwamua kutoka lindi la umaskini umeanza kuzaa matunda na kubadili maisha ya jamii hizo ikiwemo nchini Kenya. Chini ya mpango huo, UNICEF hutoa dola Ishirini kila mwezi kwa mtu aliyejiandikisha ambapo [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa unahamisha kwa muda wafanyakazi wake wasio wa lazika kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati kutokana na kuzorota kwa usalama na kutotekelezwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, licha ya waasi wa kikundi kiitwacho SELEKA kudai kuwa watasitisha na kuacha kusonga kuelekea mji mkuu Bangui. Taarifa kutoka ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa [...]
27/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Harakati za viwanda kujaribu kuhifadhi mazingira kwa kutumia mabaki ya malighafi za bidhaa zake kuzalisha bidhaa nyingine zinazidi kushika kasi, na viwanda kuwa mifano kwa viwanda vingine kama njia mojawapo ya kuhifadhi mazingira huku zikijiibulia huduma zingine. Miongoni mwa viwanda hivyo ni kile cha sukari cha Mumias nchini Kenya ambacho sasa kinazalisha umeme kwa kutumia [...]
26/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kundi la watu mashuhuri, wakiwemo Rais wa zamani wa Ufaransa Jacques Chirac na Balozi wa mfuko wa Danielle Mitterrand, Valérie Trierweiler ambaye pia ni rafiki wa rais wa sasa wa Ufaransa, wametoa wito kwa Umoja wa Mataifa kupitisha azimio litakaloruhusu askari wa kulinda amani wa Umoja huo huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, MONUSCO kuongezewa [...]
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamadunia, UNESCO, Irina Bokova amelaani mauaji ya mwandishi wa habari wa televisheni nchini Syria, Haidar al-Sumudi . Bi. Bokova amesema amesikitishwa na mauaji ya mwandishi huyo pamoja na mashambulizi yanayoendelea dhidi ya waandishi wa habari nchini Syria na kusema uhuru wa kujieleza ni [...]
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mpango wa mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendeleo ya Kilimo, IFAD wa kufadhili miradi ya upandaji miti nchini Kenya umeanza kuzaa matunda ambapo tangu mwaka 2005 hadi sasa zaidi ya miche Milioni Moja imepandwa katika maeneo ya vyanzo vya maji kwenye miteremko ya mlima Kenya. Miche hiyo inajumuisha miche Elfu Nne iliyopandwa na shule [...]
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kufuatia mazungumzo ya siku kadhaa, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limekalimisha sehemu kubwa ya kikao chake cha 67 kwa kupitishwa kwa azimio mbili kutoka kwa kamati za usimamizi na bajeti. Baraza hilo lenye wanachama 193 limechukua maamuzi kutokana na jinsi vile wanachama watakavyoweza kuchangia bajeti za shughuli za kulinda amani kwa muda wa miaka [...]
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ikiwa imepita kiasi cha siku 650 tangu kuanza kwa machafuko nchini Syria, idadi kubwa ya watu sasa wameingia kwenye wakati mgumu wa kusaka hali ya joto katika wakati ambapo kiwango cha nyuzi joto kikishuhudiwa kupungua. Kiwango hicho cha nyuzi joto kinatazamiwa kushuka zaidi kuanzia mwezi ujao ambao taifa hilo linakumbwa na hali mbaya zaidi ya [...]
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakimbizi wa Burundi waliokuwa wakiishi Tanzania kwa miongo kadhaa pamoja na familia zao na ambao wamerejea nyumbani baada ya amani kupatikana nchini mwao, wamekiri kushuhudia hali ya amani nchini mwao tofauti na taarifa waliozokuwa wakipata wakiwa kwenye kambi.Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (SAUTI YA ALICE KARIUKI)
26/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtendaji Mkuu wa Mkataba wa kimataifa wa udhibiti wa biashara ya viumbe vilivyo hatarini kutoweka, CITES, John Scanlon amesifu wito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kutaka uchunguzi dhidi ya madai kuwa waasi wa kikundi cha LRA wanaua tembo na kuuza meno yao kimagendo. Bwana Scanlon amesema hatua hiyo ni ya kihistoria [...]
24/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO Irina Bokova ameeleza kusikitishwa kwake na kubomolewa hivi karibuni kwa makaburi takribani matatu ya kihistoria katika mji wa Timbuktu nchini Mali. Taarifa ya UNESCO imemkariri Bi. Bokova akisema kitendo hicho kimetokea wakati shirika lake limeanza kutekeleza wajibu wake kwa wananchi wa [...]
24/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Miili ya askari wanne wa Urusi waliofariki dunia baada ya helikopta waliyokuwemo ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kutunguliwa huko jimbo la Jonglei siku ya Ijumaa imesafirishwa leo kwenda nyumbani. Ibada ya kuwaombea ilifanyika kwenye kituo cha UNMISS karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba. Naibu [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki, Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la wahamiaji, IOM hii leo limeanza tena mpango wa kuwarejesha makwao raia wa Sudan Kusini kutoka mjini Khartoum ambao maisha yao yako hatarini. IOM imesema raia hao wanaorejeshwa kwa ndege ni pamoja na wazee, wagonjwa na wengineo na mpango huo umeanza tena leo baada ya kusitishwa kufuatia kuanguka kwa ndege [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na umoja wa nchi za kiarabu, kwenye mgogoro wa Syria Lakdhar Brahimi, amesema hali nchini Syria bado inatia wasiwasi na hivyo ametaka pande husika kwenye mgogoro huo kuchukua hatua madhubuti kwa ustawi wa raia wa Syria. Bwana Brahimi amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mazungumzo [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezungumzia vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake ukiwemo ukeketwaji na kusema kuwa vitendo kama hivyo vinaweka hatarini afya za wanawake na wasichana wengi kote duniani. Amesema afya za mamilioni ya wanawake na watoto duniani kote ziko hatarini na kwamba kuendelea kwa vitendo hivyo kunavunja haki zao za [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya majina ya watu waliopendekezwa kuchukua wadhifa wa Ukurugenzi mkuu wa shirika la biashara duniani, WTO pindi Mkurugenzi Mkuu wa sasa Pascal Lamy atakapomaliza muda wake mwakani yamezidi kuongezeka baada ya Kenya kumteua Balozi Amina Mohammed kuwania nafasi hiyo. Balozi Amina kwa sasani msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia Naibu [...]
24/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nchi za Asia – Pasific zimeridhia mpango wa utekelezaji unaotumia teknolojia ya anga za juu kushughulikia majanga ya kiasili na hatimaye kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwenye ukanda huo. Makubaliano hayo yamefikiwa mwishoni mwa mkutano wa siku mbili ambapo mpango huo unataka tume ya Uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa kwa nchi za Asia [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mamia ya wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao wamekosa makwao kutokana na machafuko yanayojiri katika eneo la Mashariki mwa nchi hiyo wameanza kupokea misaada muhimu ikiwemo vifaa vya kujikimu huku wasambazaji wa huduma hizo wakikabiliana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha. Kiasi cha familia 23,000 zilizoko jimbo la Kaskazini ya Kivu, kimepatiwa vifaa vya [...]
24/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalamu mpya wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Eritrea Beedwantee Keetharuth ametaka nchi hiyo kuonyesha ushirikiano wa kushughulikia haki za binadamu nchini humo kwa mujibu wa Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. Taarifa ya ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imemkariri Bi. Keetharuth akisema [...]
21/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ulimwengu unaendelea kushuhudia dhuluma mbalimbali dhidi ya wanawake, ikiwemo ukatili, kwa madai eti ni utekelezaji wa mila na desturi za jamii husika. Mathalani ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, vipigo, uminyaji wa matiti ya watoto wa kike kama madai ya kumlinda mtoto dhidi ya kutumbukia kwenye ngono mapema na kadhalika. Moja mwa njia muafaka [...]
21/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika unaolinda amani kwenye jimbo la Darfur, nchini Sudan UNAMID, umeeleza wasiwasi wake juu ya ripoti za raia kukimbia makazi yao kutokana na mashambulio ya anga yanayodaiwa kufanywa na jeshi la Sudan na vikundi vyenye silaha huko Shangil Tobaya na Tawila kaskazini mwa Darfur. Taarifa [...]
21/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imekaribisha hatua ya bunge la Senegal ya kupitisha sheria ya kubuniwa kwa sehemu ya mahakama itakayoendesha kesi dhidi ya rais wa zamani wa Chad Hissene Habre. Ofisi hiyo inasema kuwa imekuwa ikiunga mkono jitihada za Muungano wa Afrika AU za kuhakikisha kuwepo uwajibikaji kufuatia ukiukaji wa [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika chakula la Umoja wa Mataifa WFP litarejelea shughuli za usambazaji wa chakula kwa vituo 1600 vya huduma nchini Swaziland baada ya shughuli hiyo kuvurugwa mapema mwaka huu kutokana na ukosefu wa ufadhili. Kulingana na WFP usambazaji huo wa chakula utawanufaisha mayatima 97,000 na watoto wengine 33,000 wanaotaabika. Asilimia kubwa ya watakaopokea chakula hicho ni [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la uhamiaji duniani, IOM pamoja na mashirika yake imeonyesha madhila ambayo bado yanawakumba wakazi wa Haiti kufuatia majanga ya mfululizo yaliyokumba nchi hiyo kuanzia mwaka 2010. Mathalani ripoti hiyo inaonyesha ukosefu wa ajira, watu kuendelea kuishi kwenye makazi na idadi kubwa ya kaya kuongozwa na wanawake pekee. Tupate taarifa zaidi [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa unasema kuwa kulingana na uchunguzi lililoendesha limebainisha kuwa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo pamoja na wapiganaji wa kundi la M23 walitekeleza vitendo vinavyokiuka haki za binadamu wakati wa mapigano ya kutaka kuudhibiti mji wa Goma ulio mashariki mwa nchi hiyo. Vitendo hivyo vinaripotiwa kutekelezwa kati ya tarehe 20 na 30 [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la afya duniani, WHO limesema shambulio lolote dhidi ya wahudumu wa afya halikubaliki na kwamba migogoro au mapigano yoyote hayapaswi kubughudhi huduma za afya. WHO imetoa kauli hiyo kufuatia kupigwa risasi na kuuawa kwa wafanyakazi sita waliokuwa wanaendesha kampeni ya polisi nchini Pakistan. Shirika hilo limesema vitendo hivyo vikifanyika, wanaopata madhara ni watoto na [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP litaanza kusambaza msaada wa dharura wa chakula kwa maelfu ya wakimbizi wa kipalestina waliokumbwa na mapigano kwenye kambi ya Yarmouk, iliyoko mji mkuu wa Syria, Damascus. WFP inatarajia kuwapatia msaada huo ambao ni mlo wakimbizi 125,000 wa kipalestina pamoja na raia wa Syria waliokimbia makazi [...]
21/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kwa kutambua athari za mzozo wa mali kwa amani na usalama duniani, hii leo Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha kwa kauli moja azimio ambalo pamoja na mambo mengine linataka waasi nchini humo kuvunja mara moja uhusiano na vikundi vya kigaidi ikiwemo Al-Qaida na kuthibitisha hatua hiyo. Azimio hilo pia linataka mamlaka za [...]
20/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wamemtangaza Mohamed Ibn Chambas kuwa kiongozi mpya wa UNAMID ambao ni ujumbe wa pamoja wa pande mbili hizo wa kulinda amani kwenye jimbo la magharibi mwa Sudan, Darfur. Bwana Chambas ambaye ni raia wa Ghana anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Ibrahim Gambari ambaye Katibu Mkuu wa Umoja wa [...]
20/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wanawake nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati ambao wamezingirwa na mzozo na kujikuta wakikumbwa na vitendo vya dhuluma ikiwemo kubakwa wamesema wamechoshwa na hali hiyo na sasa wanataka amani na wenzao wanaoshikiliwa na waasi waachiwe huru. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya ukatili wa ngono kwenye mizozo, Zainab [...]
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /
Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kimesema hivi sasa kinatoa hifadhi kwa raia wengi wao wanawake na watoto ambao wamekimbia mji wa WAU ulioko jimbo la Bahr el-Ghazal kutokana na mzozo juu ya makao makuu ya serikali ya mtaa. Jason Nyakundi ameandaa taarifa kamili. (SAUTI YA JASON NYAKUNDI)
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maelfu ya wapalestina kwa sasa wanaendelea kuihama Syria kufuatia kuwepo mapigano makali yaliyotokea kwenye kambi ya Yarmouk mjini Damascus. Kambi hiyo ilishambuliwa kwa mabomu na ndege za kivita za Syria siku ya Jumapili kufuata tuhuma za kuwepo kwa waasi. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestinba UNRWA linakadiria kuwa theluthi mbili [...]
20/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani mashambulizi yaliyoendeshwa na makundi yaliyojihami siku chache zilizopita kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya kati pamoja na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu unaondelea. Kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari wajumbe wa Baraza hilo pia wameelezea wasiwasi wao kutokana na hali ilivyo nchini humo [...]
20/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Watu hamsini na watano wakiwemo raia wa Somalia na Ethiopia wanahofiwa kufa baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kando mwa pwani ya Somalia siku ya Jumanne. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limesema maiti 23 wamepatikana na watu wengine 32 bado hawajulikani walipo kwa hiyo inaaminika wamezama. Watu hao walikuwa wakisafiri kwa [...]
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limekuwa na mjadala wa wazi kuhusu ujenzi wa amani baada ya migogoro ambapo Katibu Mkuu Ban Ki- Moon amesema maendeleo ya dhati yamepatikana katika ajenda ya ujenzi wa amani. Akihutubia kikao hicho, Bwana Ban amesema hata licha ya mafanikio yaliyopatikana, bado kuna changamoto lukuki. Amesema baadhi [...]
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR limeelezea wasiwasi wake kutokana na matukio ya hivi karibuni nchini Kenya ya kuuawa kwa raia pamoja na wakimbizi. UNHCR imesema inalaani mashambulizi hayo na kutoa rambirambi kwa waathirika wote, watu na serikali ya Kenya huku ikiomba serikali hiyo kuendelea kulinda haki za wakimbizi.
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mgogoro unaoendelea nchini Syria umeripotiwa kuchukua mwelekeo wa kidini ambapo baadhi ya vikundi vinalazimika kupambana ili kujilinda au kuonyesha mshikamano na moja ya pande zinazozozana katika mgogoro huo. Taarifa hizo ni kwa mujibu wa Tume huru iliyoundwa kuchunguza mzozo wa Syria ambapo imesema majeshi ya serikali na wanamgambo wenye silaha wamekuwa wakishambulia raia wa madhehebu [...]
20/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mahakama ya Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya Rwanda, imemhukumu waziri wa zamani wa nchi hiyo Augustin Ngirabatware kifungo cha miaka 35 jela baada ya kumpata na hatia ya kuhusika na mauaji ya halaiki nchini mwake mwaka 1994. Akisoma hukumu hiyo, Jaji William Hussein aliyeongoza jopo la majaji watatu amesema Ngirabatware amepatikana na hatia ya [...]
20/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya mshikamano kibinadamu hii leo na kusema mshikamano ndio njia pekee ya kutatua migogoro inayokumba dunia ya sasa yenye mwingiliano mkubwa. Ujumbe wa mwaka huu ni ubia wa kimataifa kwa ustawi wa pamoja. Amesema siku hii ni muhimu zaidi kwa [...]
20/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja mataifa kupitia msimamizi Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani, Herve Ladsous umetangaza bayana kuwepo kwa sintofahamu ya hali ya usalama huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Hali hiyo imeibuka baada ya kuondoka kwa waasi wa M23 mwanzoni mwa mwezi huu, lakini kumeripotiwa [...]
19/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amemtumia salamu za pongeza Park Geun-hye kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Korea na kuelezea utayari wa kushirikiana na serikali mpya ya nchi hiyo. Bi. Park, mtoto wa dikteta wa zamani nchini Jamhuri ya Korea Park Chung-hee, ameibuka mshidni katika uchaguzi wa Jumatano na anakuwa [...]
19/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wito wa kutaka kurejeshwa kwa haraka mchakato wa amani kati ya Palestina na Israeli umetolewa kwa nyakati tofauti hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani, kutokana na mazungumzo ya moja kwa moja kati ya pande mbili hizo kufanyika mara ya mwisho mwezi Septemba mwaka 2010. Katika mkutano wake wa [...]
19/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katika harakati za kukabiliana na vitendo viovu vinavyofanywa na kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army kwenye maeneo ya Afrika ya Kati, Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika zinatafuta fedha zaidi kutekeleza mipango yake ya kudhibiti kikundi hicho. Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika Ofisi ya Kanda ya Afrika Ya [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa tathmini yake ya mwaka huu wa 2012 unaofikia ukingoni na kuelezea kuwa ulikuwa ni mwaka uliosheheni mizozo na migogoro lakini Umoja wa Mataifa licha ya hali hiyo uliweza kuendeleza ajenda yake ya maendeleo endelevu kwa karne ya 21 huku ikiendeleza jukumu lake la kulinda amani na [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tangu kuondoka kwa waasi wa M23 kutoka mji wa Goma mapema mwezi huu, hali ya sintofahamu kuhusu usalama kwenye eneo hilo imeendelea kudumu katika mji huo mkuu wa jimbo la Kivu kaskazini. Kutokana na hali hiyo Msimamizi Mkuu wa masuala ya operesheni za ulinzi wa amani kwa Umoja wa Mataifa, Hervé Ladsous amesema MONUSCO ambacho [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP , Muungano wa Afrika AU na ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye jimbo la Darfur UNAMID wametoa mafunzo kwa maafisa wa magereza katika eneo la El Fasher kaskazini mwa jimbo la Darfur nchini Suadn kama moja ya njia ya kuboresha idara za sheria. Mwakilishi wa UNAMID Hastings [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkataba wa kimataifa wa matumizi ya vito vizito umepiga hatua baada ya kuungwa mkono na mataifa kadhaa kufuatia jitihada za majadiliano za miaka 3. Mkataba huo ambao ni umeratibiwa na kamishna ya kitaifa inayohusika na masuala ya uchumi barani Ulaya UNECE umelenga kukabiliana na uchafuzi wa hewa angani. Kwa mara ya kwanza mkataba huo uliasisiwa [...]
19/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa na washirika wa huduma za kibinadamu wametoa ombi la dola milioni 144 zitakazotumika kusaidia zaidi ya watu milioni moja nchini Haiti mwaka 2013. Ufadhili huo utayawezesha mashirika ya kutoka misaada kukabiliana na tatizo la ukosefu wa chakula, ugonjwa wa kipindupindu na hamiaji kwenye taifa hilo la Caribbean. Mratibu wa huduma za kibinadamu [...]
19/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Suala la haki za binadamu nchini Iraq bado limesalia kuwa changamoto wakati taifa hilo linaposhuhudia mabadiliko kutoka nyakati zilizokuwa na mizozo na ghasia ikielekea kwenye demokrasia na amani imesema ripoti kuhusu haki za binadamu ya shirika la Umoja wa Mataifa. Ripoti hiyo inasema kuwa suala la ghasia limesalia ajenda kuu huku idadi ya raia waliouawa [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya raia wa Syria waliopoteza makazi yao kutokanana mapigano yanayoendelea nchini mwao inatarajiwa kuongezeka na kufikia Milioni Nne katika nusu ya kwanza ya mwaka ujao. Umoja wa Mataifa unasema kuwa kati yao, Milioni Moja watakuwa wamekimbilia Jordan, Uturuki, Lebanon, Misri na idadi ya wakimbizi wa ndani itafikia Milioni Mbili. Kwa mantiki hiyo basi Umoja [...]
19/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ukuaji wa uchumi wa dunia kwa mwaka 2012 umedorora kiasi na hali hiyo inatarajiwa kuaendelea kwa miaka miwili ijayo, na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa hii leo. Rob Vos, ambaye ni Mkurugenzi wa idara ya maendeleo ya sera na upembuzi ya Umoja wa Mataifa amesema uchumi wa dunia [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Jumanne tarehe 18 Disemba limeridhia tarehe 13 ya mwezi Februari kila mwaka kuwa siku ya Radio duniani, ikiwa ni kutambua mchango wa Radio katika kurusha matangazo mbali mbali ya kuleta maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii na vile vile kwa kutambua nafasi ya Radio ya Umoja wa [...]
18/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa hii leo limeridhia azimio la shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Teknolojia, UNESCO la kutaka tarehe 13 Februari ya kila mwaka kuwa siku ya kimataifa ya Radio duniani. Tarehe 13 Februari mwaka 1946 ni siku ambayo Radio ya Umoja wa Mataifa ilianza kufanya kazi ambapo Baraza [...]
18/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya watoto na mizozo bi Leila Zerrougui amekamilisha ziara yake nchini Syria, ziara iliyomkutanisha na utawala wa nchi hiyo na makundi yaliyojihama na kujadili suala la usalama kwa watoto. Mjumbe huyo amesema kuwa kisa ambapo watoto wawili ya kipalestina waliuawa na kujeruhiwa kwenye kambi [...]
18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kumekuwa na hali ya mkwamo unaowaandama raia wa Syria katika wakati ambapo matokeo ya mzozo huo umeathiri pia ustawi jumla ya wale wanaotajwa wakimbizi wa Kipalestina. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi wa Palestina UNRWA, limeanzisha juhudi ya usambazaji wa huduma za kibinadamu kwa zaidi ya wakimbizi 150,000 walioko katika kambi ya Yarmouk. [...]
18/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Uzalishaji wa mazao yatokanayo na misitu unaarifiwa kusuasua tangu kushuhudiwa kwa mkwamo wa uchumi wa dunia, huku mataifa yaliyoko katika kanda ya Asia-Pacific ndiyo yakishika nafasi ya kwanza. Hata hivyo China ndiyo iliyotajwa kuwa ndiyo inayofanya vizuri zaidi ikilinganishwa na mataifa mengine duniani. Ripoti mpya iliyotolewa na shirika la chakula na kilimo duniani FAO [...]
18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati Somalia inajenga upya taasisi zake za ulinzi na usalama, serikali ya nchi hiyo imetakiwa kuhakikisha kuwa vikosi binafsi vya ulinzi vinaongozwa kwa kanuni na sheria na havigeuzwi kuwa mbadala wa vikosi thabiti vya polisi. Hilo ni tamko lililotolewa na kikundi cha wataalamu wanaochunguza matumizi ya mamluki waliofanya ziara nchini Somalia kwa siku saba wakiongozwa [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema hali ya kibinadamu nchini Syria inazidi kuzorota ambapo mahitaji ya chakula yanazidi kuongezeka, halikadhalika idadi ya watu wanaopoteza makazi yao. Msemaji wa WFP Elizabeth Byrs amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa hivi sasa wanahudumia watu Milioni Moja na Nusu kwa mwezi nchini Syria. Hata hivyo [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai, ICC imeamuru kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa makosa ya uhalifu wa kivita dhidi ya binadamu, Mathieu Ngudjolo Chui baada ya kumuona kuwa hana hatia. Uamuzi huo umepitishwa kwa kauli moja na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Bruno Cotte kutoka Ufaransa ambapo wamesema upande wa mashtaka umeshindwa [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa hali ya usalama kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mugunga 3 karibu na mji wa Goma nchini Jamhuri ya Kidemeokrasi ya Congo ni ya kutia wasi wasi. Akiongea na waandishi wa habari mjini Geneva msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa wanajeshi na [...]
18/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Karibu wanawake na wasichana 400 walibwakwa kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wakati wa mapigano ya hivi majuzi kweneye mji wa Goma. Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa huduma inatolewa kwa wanawake 278 na wasichana 117 waathiriwa wa dhuluma za kimapenzi. UNICEF inasema kuwa wanawake [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Jopo la wataalamu wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, wataalamu wa haki za wahamiaji na Muungano wa nchi za bara la Amerika limeelezea wasiwasi wake kuhusu tabia ya baadhi ya nchi kuchukulia kitendo cha mtu kukosa nyaraka rasmi za ukaazi kama uhalifu. Katika taarifa ya pamoja kuadhimisha siku ya kimataifa [...]
18/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya wahamiaji hii leo, shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limetaka jumuiya ya kimataifa hususan nchi zinazotoa au kupokea wahamiaji kutambua athari za majanga na mizozo kwa wahamiaji. Msemaji wa IOM Jean Phillip Chauzy ametolea mfano wahamiaji Laki Mbili nchini Libya kutoka nchi maskini ambao mwaka 2011 walijikuta katika mazingira [...]
18/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Hatimaye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amerejea katika ofisi yake iliyoko kwenye jengo kuu la umoja huo mjini New York, Marekani baada ya ukarabati uliodumu kwa takribani miaka mitano. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuingia katika ofisi yake hiyo, Bwana Ban amesema ukarabati huo ni wa kihistoria kwa kuwa umezingatia [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Hali ya usalama katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini imeripotiwa kuwa ni ya wasiwasi baada ya waasi wa kikundi cha M23 kuonekana katika viunga vya mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martini Nesirky amewaambia waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo [...]
17/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya ya shirika la afya duniani, WHO kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa mwaka 2012 imeonyesha kupungua kwa ufadhili katika mipango ya vita dhidi ya ugonjwa huo uliosababisha vifo vya watu takribani Laki Sita na Elfu Sitini duniani kote. Idadi kubwa ya vifo hivyo ni vya watoto wenye chini ya umri wa miaka mitano. Hata [...]
17/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq, Martin Kobler, ameshutumu vikali msururu wa mashambulio ya jana na leo yaliyotokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 44 na wengine 77 wamejeruhiwa. Habari zinasema katika shambulio la leo alfajiri kaskazini mwa nchi hiyo lililolenga askari wa jeshi la Iraq na raia, watu [...]
17/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema anasikitishwa na mwendelezo wa ghasia nchini Syria katika siku za karibuni na hatari kubwa inayokabili raia kwenye maeneo ambako kuna mapigano. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza masikitiko hayo huku akishutumu mashambulizi ya silaha kwenye maeneo ya raia ambapo amerejelea kauli yake ya kutaka pande [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku asilimia 72 ya wakazi wa Sudan Kusini wakiwa chini ya umri wa miaka 30, Shirika la Umoja wa Mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni, UNESCO linaeleza kuwa ni bayana kwamba hatma ya taifa hilo iko mikononi mwa vijana. Ili kuweza kulea kizazi kipya balozi wa uhusinao mwema wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Naibu mkurugenzi mkuu kwenye masuala ya usalama wa nuklia kwenye Shirika la kudhibiti nishati ya atomic duniani IAEA Denis Floy amesema kuwa mkutano ambao umekamilika umetoa fursa nzuri wa kubadilishana ujuzi kutokana na ajali ya kituo cha Fukushima Daichi nchini Japan na pia kutoa mwelekeo wa kuwepo jitihada za kimataifa za kuhakikisha kuwepo usalama wa [...]
17/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu na kusimamia ulinzi kwa wakimbizi wa Kipalestina, lUNRWA Filippo Grandi ameiomba Syria na pande zote katika mzozo nchini humo kuhakikisha wakimbizi wa Syria, popote pale walipo nchini humo wanapatiwa ulinzi. Ombi la Grandi linafuatia picha zilizochapishwa na mashirika mbali mbali ya habari zinazoonyesha hali ya [...]
17/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna ya Umoja wa Mataifa juu ya wakimbizi António Guterres ametangaza kuanzishwa kwa kituo cha pamoja kitaratibu misaada ya kibinadamua kwa mamia ya wananchi wanaokimbia mapigano nchini Syria ambao hadi sasa wamefikia 250,000 waliopata hifadhi nchini Jordan. Kituo hicho ambacho kitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja baina ya Umoja wa Mataifa na Jordan kinalenga kukabiliana na [...]
17/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la afya duniani, WHO limesema dola Bilioni Tano zinahitajika kila mwaka kwa kipindi cha muongo mmoja ujao ili kuhakikisha tiba dhidi ya Malaria inapatikana duniani kote. Hata hivyo WHO imesema mpaka sasa ni nusu tu ya kiwango hicho ndicho kinapatikana na hivyo kukwamisha harakati za kupambana na ugonjwa huo. Dkt. Richard Cibulskis mtaalamu kutoka [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu, OCHA limeeleza kuwa kati ya dola Bilioni Nane na Nusu zilizoombwa kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2013, takribani dola Bilioni Moja ni kwa ajili ya Sudan pekee. Sudan inahitaji fedha hizo kwa ajili ya miradi 364 ya misaada ya kibinadamu kwa mwaka [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Afya duniani WHO, limechapisha ripoti yake ya mwaka 2012 inayoaangazia tatizo la Malaria ambayo imesema kasi ya kukabiliana na tatizo hilo imekosa msukumo na kushuka kiasi. Ripoti hiyo ambayo imezinduliwa katika mji Mkuu wa Liberia, Monrovia na rais wa taifa hilo, Ellen Johnson Sirleaf, imeonyesha kushuka kwa jitihada za kukabiliana na kasi ya ugonjwa [...]
17/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Sauti yangu ina nafasi! Ni ujumbe wa siku ya kimataifa ya haki za binadamu iliyoadhimishwa tarehe 10 Desemba mwaka huu, siku ambayo miaka 64 iliyopita lilipitishwa tamko la kimataifa la haki za kibinadamu. Mwaka huu ujumbe huo unatoa fursa kwa makundi yote hususan wanawake, vijana, makundi madogo, walemavu, wapenzi wa jinsia moja, mashoga na hata [...]
14/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN mjini New York, Marekani umemalizika kwa mataifa 12 kuitikia wito wa shirika hilo wa kuzitaka nchi dunia kuongeza juhudi za kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Kupitia mpango mpya, COMMIT, nchi hizo ikiwemo Togo, Ufaransa, Marekani [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea zaidi ya dola 700,000 kufadhili shughuli za misaada kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha nchini Ufilipino, misaada ambayo ni pamoja na huduma za afya na malazi. Kulingana na ripoti IOM kwa ushirikiano na idara ya kijamii na maendeleo DSWD juma hili ilitoa msaada wa makao ya dharura kwa familia [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baada ya wiki mbili za majadiliano, huko Dubai, wajumbe wa mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU wamekubaliana kuhusu mkataba mpya wa mawasiliano ya simu. Taarifa ya ITU inasema madhumuni ya mkataba huo mpya ni kuwezesha muunganiko wa kirahisi zaidi wa dunia kwa kutumia teknolojia ya kisasa habari na mawasiliano, ICT. ITU [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wajumbe zaidi ya 160 waliokuwa wanakutana huko Doha, wamekamilisha hatua ya kwanza muhimu ya uandikaji wa rasimu ambayo inakusudia kutumika kwa ajili ya kuyafanyia marekebisho miongozo ya mawasiliano duniani. Kukamilika kwa rasimu hiyo kutafanikisha mageuzi ya sheria ambayo sasa itaruhusu uhuru wa kusafirisha taarifa duniani kote bila vikwazo vyovyote. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Jopo la wataalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa limeonyesha wasiwasi kuhusu mwelekeo wa rasimu ya katiba nchini Misri na kuitaka serikali ya nchi hiyo kuhakikisha mwishowe Katiba inakuwa si ya kibaguzi bali inalinda usawa na kuendeleza haki za wanawake. Mmoja wa wataalamu hao Kamala Chandrakirana amesema mpaka sasa fursa muhimu ya [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeeleza kusikitishwa kwake na kutokuwepo kwa maendeleo ya dhahiri ya kurejesha utawala wa kikatiba nchini Guinea-Bissau. Katika taarifa yake, Baraza hilo imesema wajumbe wake 15 wanaamini kuwa utuliv unaweza kurejea kupitia mchakato utakaokubaliwa na pande zote kwa kuzingatia mashauriano ya dhati. Wajumbe hao wamerejelea azimio namba 2048 la [...]
14/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kikundi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kinacholinda amani huko Darfur, UNAMID kimekabidhi mahakama ya kijiji huko Tawilla, kaskazini mwa Darfur. Mahakama hiyo yenye lengo la kurahisisha utekelezaji wa shughuli za mahakama kwenye eneo hilo, ni sehemu ya miradi ya UNAMID ya kuleta mabadiliko yanayoonekana haraka, kwa lengo la kuleta amani [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linasema kuwa watoto waliobakia bila makazi katika maeneo yaliyokumbwa na kimbunga huko Ufilipino wako hatarini kunyanyaswa na kutumikishwa. UNICEF inasema licha ya kwamba kazi nzuri imefanyika kukabiliana na madhara ya kimbunga, lakini mahitaji muhimu ya watoto hayatiliwi maanani na hivyo kuwaweka hatarini zaidi kudhalilika ikiwemo kusafirishwa [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kiwango cha malipo ya ujira nchini China kimeongezeka mara tatu kati ya mwaka 2000 na 2010 na hivyo kuonyesha dalili za uwezekano wa kuanza kutoweka kwa dhana iliyozoeleka ya ujira mdogo miongoni mwa wachina. Ripoti ya mwaka huu ya ILO kuhusu malipo ya ujira imejumuisha viwango vya ujira katika mashiriak ya kiserikali na makampuni madogo [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limepokea dola 700,000 pesa za Canada kufadhili shughuli za misaada kwa waathiriwa wa kimbunga Bopha. Kulingana na ripoti IOM kwa ushirikiano na idara ya kijamii na maendeleo DSWD juma hili ilitoa msaada wa makao ya dharura kwa familia 600 au watu 30,000 ambao wamekuwa wakiishi nje tangu tufani hiyo [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mdororo wa kiuchumi duniani unazidi kuendelea kuathiri maendeleo ya nchi za Asia na Pasifiki ambapo taarifa hizo ni kwa mujibu wa makadirio mapya ya Tume ya Umoja wa Mataifa ya Maendeleo ya uchumi na kijamii kwa nchi za Asia-Pasifiki, ESCAP. Makadirio hayo yaliyotolewa leo huko Thailand yanaonyesha kuwa ukuaji uchumi katika nchi tajiri umeendelea kudorora [...]
14/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takwimu za mwaka 2012 zilizochapishwa hii leo za shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuongezeka kwa mchango kutoka kwa nchi zinazoendelea kwa uchumi wa dunia kutokana hasa na uundaji wa meli na vifaa vya electroniki. Yakiongozwa na mataifa yaliyostawi ya Asia, mataifa yanayoendelea yameongeza mchango wao kwa mauzo ya nje ya [...]
14/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umetangaza ombi la dola Bilioni 8.5 kwa ajili ya operesheni zake za misaada ya kibinadamu kwa mwaka 2013. Fedha hizo zinalenga kuwahudumia watu Milioni 51 kutoka nchi 16 duniani ambao wanahitaji misaada ya kibinadamu. Katika usambazaji wa huduma hizo, jumla ya mashirika 520 ya misaada yatashirikiana na Umoja wa Mataifa kuwapatia misaada [...]
14/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii duniain kote ikiwemo nchi zinazoendelea. Inaelezwa kuwa matumizi ya simu ikiwemo zile za mkononi ambazo kwa sasa zinaweza kutuma picha na hata sauti, zimeweza kuwa mkombozi kwa mwananchi wa kawaida. Mathalani wapo waliofungua vioski kwa ajili ya kutoa huduma za kutuma [...]
13/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umelitaka jeshi la Sudan Kusini kujizuia pindi linapokabiliana na raia. Kikundi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko Sudan Kusini, UNMISS kimetoa taarifa hiyo kufuatia matukio ya hivi karibuni ya mapambano kati ya waandamanaji na polisi yaliyosababisha vifo vya raia Tisa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Taarifa hiyo imesema kwa sasa [...]
13/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Majaji katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC, wametupilia mbali madai yaliyotolewa na upande wa utetezi wa aliyekuwa rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo waliodai kuwa majaji hao hawakustahili kuendesha kesi hiyo. Mawakili wanaomtetea Gbagbo waliwalisiha rufani kwenye mahakama hiyo wakidai kuwa majaji wanaoendesha kesi hiyo wanakosa nguvu za kisheria [...]
13/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Zaidi ya watu 400 ikiwemo viongozi wa dini na wataalamu wa imani wamekusanyika mjini Geneva ambako wanajadiliana kuhusu tofauti za kiimani zinavyoweza kutoa mchango kuwasaidia watu wanaoandamwa na matatizo ikiwemo wakimbizi. Mkutano huo wa siku mbili unashabaha ya kuangalia kwa kiasi gani pamoja na kuwepo kwa tofauti za kidini, lakini bado imani hizo zikawa katika [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama hii leo limepokea ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja huo Ban Ki Moon kuhusu Sudan ambayo pamoja na mambo mengine imeelezea hatua zilizofikiwa katika kuwafikisha mbele ya sheria watuhumiwa vitendo vya uhalifu huko Darfur. Ripoti hiyo imewasilishwa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, Fatou Bensouda ambaye [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, Ertharin Cousin, amehitimisha ziara yake ya siku mbili huko Saudi Arabia na kusema kuwa ushirikiano kati ya pande mbili hizo umesaidia kuokoa maisha ya mamilioni ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kote. Katika mazungumzo yake na Mwanamfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud, Bi Cousin amesema [...]
13/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya watalii waliotembelea dunia hii leo imetimia Bilioni Moja na kuweka rekodi mpya kwenye utalii wa kimataifa sekta inayochangia nafasi moja kwa kila ajira 12 duniani. Kwenye tarehe ya kuadhimisha mtalii nambari bilioni moja ambayo ni leo tarehe 13 shirika la utalii duniani UNWTO limetaja hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa na watalii kuhahakikisha kuwa safari [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya uchumi na kijamii, Wu Hongbo amesema kazi zaidi inahitajika kufanyika kufikia usawa wa kijinsia licha ya hatua zilizofikiwa kutokana na utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia. Akizungumza katika mahojiano mjini Geneva, Uswisi, kabla ya mjadala kuhusu mbinu za kuimarisha usawa wa kijinsia na [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kaimu Mkuu wa kikundi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kinacholinda amani huko Darfur, UNAMID, Aïchatou Mindaoudou amesema ushirikiano miongoni mwa pande zote husika kwenye eneo hilo ndio njia pekee ya kuwezesha ulinzi wa raia. Bi. Mindaoudou amesema hayo baada ya ziara yake ya siku mbili katika maeneo ya Kusini na [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeongeza muda wa kuhudumu kwa majaji watano kwenye mahakama ya kimataifa inayosikiliza kesi za uhalifu wa kivita nchini Rwanda ICTR kwa lengo la kuiwezesha mahakama hiyo kumaliza kazi yake. Mahakama hiyo yenye makao yake mjini Arusha nchini Tanzania ilibuniwa baada ya kutokea mauaji ya halaiki nchini Rwanda ambapo [...]
13/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yameripotiwa kusaidia kuimarisha sekta ya utoaji huduma mbali mbali nchini Tanzania, ikiwemo za afya na kiuchumi, na hiyo ni kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo Profesa John Nkoma ambaye yuko Dubai, Falme za kiarabu akishiriki mkutano wa shirika la kimataifa la mawasiliano ya simu, ITU. [...]
13/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wajumbe wa Baraza la Usalama leo wamefanya mashauriano kuhusu hofu na wasiwasi ulioibuka kufuatia kitendo cha Jumanne cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK kurusha roketi kwa kutumia teknolojia ya makombora ya masafa marefu ambapo wameshutumu vikali kitendo hicho. Rais wa Baraza hilo Mohammed Loulichki amewaambia waandishi wa habari baada ya mashauriano hayo [...]
12/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa vitendo vya usafirishaji watoto duniani vimeongezeka ambapo asilimia 27 ya waathirika wa vitendo vya usafirishaji wa binadamu duniani kote ni watoto. Ripoti hiyo ni matokeo ya utafiti uliofanywa kati ya mwaka 2007 na 2010 na ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na udhibiti wa madawa ya kulevya [...]
12/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI UNAIDS imesema kuwa dunia inaweza kupiga hatua kubwa kukabiliana na tatizo la kuenea kwa virusi vya ugon jwa huo iwapo wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi wakapewa nafasi ya kusikika. Ripoti hiiyo yenye kichwa cha habari kisemacho, sauti ya wanawake, imeorodhesha mafanukio [...]
12/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwenyekiti wa Kamati ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za watoto Jean Zermatten, amelaani na vikali tukio la kunyongwa kwa mtoto mmoja wa kike Hind Al-Barti akisema kuwa kitendo hicho kilichotekelezwa mwezi huu mjini Sana'a nchini Yemen ni ukiukwaji mkubwa wa mikataba ya Umoja wa Mataifa. Duru zinasema kuwa mtoto huyo alikuwa na umri [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Chama cha mabunge duniani, IPU kimesema harakati za kupigania demokrasia nchini Misri hazitakuwa na ukomo bila ya kuwepo kwa katiba inayokubaliwa na wananchi wote na ambayo pia itawahakikishia haki na usawa. Rais wa IPU Abdelwahad Radi amekaririwa akisema hayo huku akilaani matukio ya siku za karibuni ya ghasia na vifo nchini Misri na kitendo cha [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ugonjwa wa Kipindupindu umeendelea kuwa tishio nchini Haiti hali iliyolazimu Umoja wa Mataifa kutoa nyongeza ya dola Milioni 23 zaidi kusaidia vita dhidi ya ugonjwa huo. Nyongeza hiyo inajazia kiasi cha dola Milioni 118 ambazo Umoja wa Mataifa umeshatumia hadi sasa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa huo nchini Haiti. Nigel Fisher ni Naibu mwakilishi [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu unyanyasaji wa kingono kwenye migogoro, Hawa Bangura amehitimisha wiki moja ya ziara yake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati na kueleza kuwa unyanyasaji wa kingono bado ni tatizo dhahiri nchini humo hasa maeneo yanayodhibitiwa na vikundi vya kisiasa au kijeshi. Amesema kwa muda wote aliokuwepo [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya elimu Kishore Singh ametoa wito kwa serikali kote duniani kuheshimu na kutekeleza wajibu wao wa kulinda haki ya elimu hasa kwa wasichana ambao wamepitia maisha magumu na walionyimwa elimu. Bwana Singh aliyasema alipohudhuria warsha moja mjini Paris yenye kauli mbiu "Mtetee malala au msichana, Elimu ni [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amelaani kitendo cha Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK cha kurusha roketi hapo jana kinyume na azimio la Umoja huo. Msemaji wa Umoja wa Mataifa amemkariri Bwana Ban akisema kuwa ni jambo la kusikitisha kuwa kitendo hicho kimekiuka wito wa jumuiya ya kimataifa na azimio [...]
12/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wafadhili wamejitolea kuchanga jumla ya dola milioni 384 ambazo zitafadhili shughuli za dharura kuhudumia mamilioni ya watu wanaoathiriwa na majanga kufuatia ombi lililotolewa na Umoja wa Mataifa CERF. Akihutubia mkutano CERF uliondaliwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alimshukuru kila mmoja ambaye anajitolea kufadhili kuhakikisha [...]
12/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Balozi mwema wa Umoja wa Mataifa Yvonne Chaka Chaka ambaye yuko mjini New York Marekani kushiriki tukio la ngazi ya juu la nafasi ya uongozi katika vita dhidi ya ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsi moja au waliobadili jinsi zao amesema ni wakati muafaka serikali zinazobagua au kuhukumu watu hao zitajwe na ziabishwe kwa kuwa [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umaskini pamoja na mila na desturi ni baadhi ya mambo yanayosababisha usafi duni miongoni mwa nchi maskini. Usafi huu duni unamulika zaidi matumizi ya vyoo salama ambapo inaelezwa kuwa kutokana na baadhi ya mila baadhi ya watu wanalazimika kujisaidia haja kubwa vichakani na hivyo kuhatarisha kuenea kwa magojwa kama vile kipindupindu. Shirika la afya duniani, [...]
11/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema anakwazika na mazingira yaliyosababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Mali, Cheick Modibo Diarra huku akitaka jeshi liache kuingilia masuala ya kisiasa na uongozi wa Mali umalize mivutano yote kwa njia ya amani.Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akieleza kuwa matukio ya hivi karibuni huko Mali yanaonyesha [...]
11/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani kitendo cha jeshi nchini Mali kumkamata Waziri Mkuu wa nchi hiyo Cheik Modibo Diarra na kusababisha kujiuzulu kwa serikali. Taarifa hiyo imesema kitendo hicho ni kinyume na maazimio ya Baraza hilo yanayolitaka jeshi hilo lisiingilie kazi ya mamlaka za mpito nchini Mali. Kwa kauli moja [...]
11/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Milima ni tegemeo la wakazi wa dunia kwa shughuli na huduma mbali mbali ikiwemo maji ya kunywa, umwagiliaji, shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii na kadhalika. Hata hivyo maendeleo ya binadamu yamekuwa kikwazo kwa milima kuweza kutoa huduma hizo na hata kuhatarisha maisha ya wakazi au jamii za milimani. Katika siku ya kimataifa ya milima duniani [...]
11/12/2012 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wanawake wanakabiliwa na ukosefu wa ajira kwa viwango vikubwa zaidi ya wanaume kote duniani, huku matarajio ya hali hiyo kurekebishwa yakiwa adimu katika miaka ijayo, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Ajira Duniani, ILO. Ripoti hiyo ya ILO kuhusu mienendo ya kimataifa kuhusu wanawake mwaka 2012, inaangalia mapengo yaliyopo ya kijinsia katika nafasi za [...]
11/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema shule 250 zilizokuwa zinatumika kuhifadhi wakimbizi wakati wa mzozo huko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC zimepora vifaa au zimeharibiwa na hivyo kufanya idadi ya shule zilizoathirika na mzozo huo kufikia 600. Ripoti ya UNICEF inasema kuwa takribani wanafunzi 240,000 wameshindwa kwenda shule [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ofiki ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa imeelezea wasi wasi wake kutokana na ghasia zilizoshuhudiwa hivi majuzi kati ya wanafuzni na polisi mjini Khartoum nchini Sudan. Habari zinasema wanafunzi waliandamana kwa siku tatu mfululizo wakilalamikia vifo vya wanafunzi wannne wa chuo cha El- Gezira kilicho kati kati mwa Sudan. Hii ni baada ya [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika afya duniani WHO Jumatatu hii linatarajiwa kuzindua ripoti kuhusu ugonjwa wa Malaria duniani. Ripoti hiyo inaangazia jitihada zinazondelea za kupambana na ugonjwa wa Malaria na athari za kupungua kwa ufadhili kwenye vita dhidi ya ugonjwa huo. Ripoti hiyo pia inaonyesha hatua zilizopigwa katika kutimizwa kwa lengo la kupunguza ugonjwa wa Malaria kote dunaini kwa [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idadi ya raia wa Syria waliokimbia na kuingia nchi majirani kwa sasa imepita watu nusu milioni kwa mujibu wa Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR. UNHCR inasema kuwa karibu wasyria 510,000 wamesajiliwa au wanaendelea kusajiliwa nchini Lebanon, Iraq, Uturuki na Kaskazini mwa Afrika. UNHCR inasema kuwa chini ya nusu ya wakimbizi waliosajiliwa [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya kisayansi na Taaluma ya mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi Richard Muyungi amesema hali ya milima na maisha ya wakazi wake iko hatarini zaidi hivi sasa kutokana na shughuli za binadamu zinazosababisha mabadiliko ya tabia nchi. Akizungumza na Radio ya Umoja wa Mataifa kuhusu siku ya [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limewarejesha makwao kwa ndege raia 210 wa Ethiopia waliokuwa wamekwama huko Yemen baada ya kushindwa kuingia Saudi Arabia kutafuta ajira. IOM inasema imegharimu dola Milioni Mbili nukta Moja ambazo ni msaada kutoka Uholanzi kusafirisha raia hao ambao wanafikisha idadi ya raia 9,500 wa Ethiopia waliorejeshwa nyumbani kutoka Yemen kwa [...]
11/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa na washirika wake wa kibinadamu leo wametoa ombi la dola milioni 65 kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ili kusaidia mamilioni ya watu walioathirika kutokana na Kimbunga Bopha huko Ufilipino. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), fedha zitatumika katika Mpango unaojulikana kama Action Recovery Plan [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki, Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon ametaka kuongezwa kwa shime zaidi duniani ili nchi zote zitie saini na kuridhia mktaba wa kimataifa wa sheria ya bahari, ambao mara nyingi hutambuliwa kama Katiba ya masuala ya bahari. Akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika maadhimisho ya miaka 30 tangu kupitishwa kwa mkataba [...]
10/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Jan Eliasson aliyeko ziarani nchini Lebanon ametembelea kikosi cha muda cha kulinda amani nchini humoUNIFIL na kusema kuwa ushirikiano kati ya kikosi hicho na majeshi ya Lebanon, LAF umeleta amani ya aina yake Kusini mwa Lebanon. Bwana Eliasson ametoa kauli hiyo baada ya kupatiwa maelezo ya operesheni za [...]
10/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katika kilele cha kampeni ya siku 16 ya kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia inayoenda sambamba na siku ya haki za binadamu hii leo, maafisa wa Umoja wa Mataifa wametaja ujumbe unaozingatiwa wakati huu ambao ni pamoja ukweli, haki na uwajibishwaji wa wale wanaokiuka haki hizo. Maeneo yaliyokumbwa na machafuko ya vita ndiyo yanayolengwa [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huko Darfur, Sudan, siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia zimefikia kilele leo ambayo ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu, ambapo kampeni ya kupinga vitendo hivyo iliratibiwa na kikundi cha pamoja cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika cha kulinda amani kwenye eneo hilo, UNAMID. Kampeni ilianza tarehe 25 mwezi [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, leo limefanya hafla ya kumuunga mkono msichana wa Kipakistani, Yousufzai Malala, na elimu ya mtoto wa kike. Hafla hiyo ambayo imeandaliwa na UNESCO pamoja na serikali ya Pakistan, imefanyika kwenye makao makuu ya UNESCO mjini Paris, Ufaransa, sambamba na siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Dhamira ya [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon amesema hali ya tahadhari inazidi kujidhirisha kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika na hivyo ni muhimu hatua za haraka zikachukuliwa kukabiliana na hali hiyo. Bwana Ban ametoa kauli hiyo leo mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani ambalo limekuwa na mjadala [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takwimu za hivi karibuni za shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU, kuhusu hali ya teknolojia duniani zinaonyesha kuwa mwanzoni mwa mwaka 2012, kulikuwa na nchi saba ambako umiliki wa simu za mkononi ulizidi asilimia 200, ikimaanisha kuwa kila mtu alikuwa na zaidi ya simu mbili. Uchina ndiyo nchi ya kwanza duniani kuwa na watu [...]
10/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi pillay ameshutumu kuendelea kutengwa kwa wanawake na makundi mengine madogo kukosa kushirikishwa kwenye masuala ya umma moja kwa moja au kupitia waakilishi wao. Pillay amesema kuwa kuwatenga wanawake hakuwanyimi tu haki zao za binadamu lakini pia fursa ya kujenga maisha yao ya baadaye. Akiongea mjini [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la kazi duniani ILO Guy Ryder ameelezea wasi wasi wake kutokana na matukio ya hivi majuzi ambayo yameshuhudiwa nchini Tunisia hasa ghasia zinazoendeshwa dhidi ya viongozi wa vyama vya wafanyikazi na ofisi za chama cha wafanyikazi nchini Tunisia (UGTT). Bwana Ryder amesisitiza kuwa mashirika ya wafanyikazi na yale ya waajiri hayawezi [...]
10/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, amesema kadri ambavyo nchi zinajizatiti kufikia malengo ya maendeleo ya milenia suala la kupambana na rushwa linakuwa ni la muhimu kuliko wakati wowote. Amesema hayo katika ujumbe wake wa siku ya kupambana na rushwa hii leo tarehe Tisa Disemba na kusema kuwa gharama ya rushwa inathibitishwa siyo [...]
09/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limepatiwa mapendekezo ya awali ya kile ambacho kinapaswa kufanywa ili kuimarisha uwezo wa kikosi cha umoja huo kinacholinda amani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, MONUSCO, suala ambalo linatokana na azimio 2076 lililopitishwa mwezi uliopita na baraza hilo. Azimio hilo lilipitishwa baada ya waasi wa [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye yuko ziarani nchini Uturuki, hii leo ametembelea kambi ya Islahiye nchini humo inayohifadhi wakimbizi wa Syria na kuelezea kushtushwa na kuguswa na kwake na simulizi kutoka kwa wakimbizi hao wakiwemo watoto. Akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara kwenye kambi hiyo iliyoko jimbo la Gaziantep, nchini humo, [...]
07/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Siko seli au seli mundu ni miongoni mwa magonjwa yanayoendelea kutikisa nchi mbali mbali duniani ambapo kila mwaka watoto Laki Tatu huzaliwa na ugonjwa huo wa kurithi, na hizo ni takwimu za Shirika la afya duniani, WHO. Kati ya hao, asilimia 80 wanatoka barani Afrika, ambako Tanzania inashika nafasi ya nne kwa kuwa na idadi [...]
07/12/2012 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti ya shirika la kazi Ulimwenguni ILO imeonyesha kuwepo kwa ongezeko ndogo la ukuaji wa ujira na wakati huo hali katika nchi zilizoendelea siyo ya kuridhisha licha maeneo hayo kushuhudia kuanza kuimarika kwa hali ya uchumi baada ya kukubwa na misuko suko ya kuanguka kwa uchumi. Ripoti hiyo ya mwaka 2012-2013 iliyotolewa leo inaonyesha kuwa [...]
07/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Takribani watu Laki Tatu na Nusu wanaishi katika vituo vya hifadhi huko Mashariki mwa kisiwa cha Mindanao nchini Ufilipino baada ya kimbunga Bopha kuharibu makazi, mali na miundombinu pamoja na kusababisha majeruhi na vifo vya watu takribani 500. Shirika la kimataifa la Uhamiaji IOM linasema kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka na kiwango cha uharibifu [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amewasili nchini Uturuki ambako anatarajiwa kufanya mashauriano na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Tayyip Erdogan na Waziri wa Mambo ya Nje, Ahmet Davutoglu. Katika ziara hiyo, Bwana Ban anatarajiwa kuzuru baadhi ya kambi za wakimbizi wa Syria ambao wamekimbilia usalama wao nchini Uturuki, kufuatia machafuko yalodumu miezi [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa kupitia sekretarieti yake ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kushirikiana na Kongamano la kidunia la uchumi, WEF wamezindua mpango mpya ujulikanao kama Msukumo wa mabadiliko,uwekezaji fedha katika vitegauchumi rafiki kwa mazingira. Ushirikiano huo umetangazwa huko Doha, Qatar ambako mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya Tabia nchi umemalizika leo na lengo la mpango [...]
07/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katika muktadha huo, mkuu wa Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA Valerie Amos yuko nchini Myanmar kutathmini hali ya kibinadamu nchini humo pamoja na athari za mizozo kwenye majimbo ya Kachim na Shan Kaskazini ambayo yamewalazimu watu 75,000 kukimbia makwao tangu kuanza kwa mapigano mwaka 2011. Amos pia atatathmini athari [...]
07/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kampeni ya dharura ya kutoa chanjo kwa sasa inaendelea nchini Syria kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa surua na polio ikiwa inawalenga watoto milioni 1.4. Kampeni hiyo inaongozwa na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF na jumla ya chanjo milioni 1.5. UNICEF inasema kuwa hakujakuwa na hakikisho kutoka kwa pande zinazozozana iwapo [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea wasi wasi wake kutoakana na kunelea kwa kizozo na mauaji kwenye maanbamano ya kupinga katiba nchini Misri ambayo inatarajiwa kuadhinishwa tarehe 15 mwezi huu. Bi Pillay amekaribisha wito wa rais Muhammed Morsi wa kutaka kufanyika kwa mazungumzo lakini akajutia kwamba hakuna hatua yoyote [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Idara ya mikasa na masuala ya dharura ya Shirika la Kimataifa la Atomiki, IAEA, imesema inawasiliana na mamlaka husika nchini Japan kufuatia tetemeko la ardhi lililopima kiwango cha 7.3 kwenye chombo cha kupima ukubwa wa tetemeko la ardhi. IAEA imesema viwanda vya nguvu za nyuklia katika maeneo ya karibu na uti wa tetemeko hilo vimeripoti [...]
07/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kampeni ya dharura ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya Manjano inaendelea huko Darfur nchini Sudan kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo. Shirika la afya duniani, WHO limesema mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo Darfur ni mkubwa kuwahi kutokea sehemu yoyote duniani kwani watu 165 wamefariki dunia hadi sasa tangu mlipuko wa [...]
07/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Miezi sita baada ya ghasia za wenyewe kwa wenyewe kuzuka katika jimbo la Rakhine magharibi mwa Myanmar, yapata watu 115, 000 walolazimika kuhama makwao bado wanaishi katika mazingira yenye matatizo, kwa mujibu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR. Shirika hilo limesema limesambaza vifaa vya misaada kwa takriban thuluthi mbili za jamii [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM limepokea dola Elfu 55 kutoka shirika la maendeleo la Uswisi, SDC kwa ajili ya kuanza kazi ya ujenzi wa makazi ya dharura kwa watu 800 waliopoteza makazi yao huko Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kideomokrasi ya Congo, DRC. Ujenzi wa makazi hayo unafuatia watu hao kukimbia makwao kutokana [...]
07/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya watu, majeruhi na uharibifu wa mali na miundombinu kutokana na kimbunga Bopha au Pablo kilichokumba eneo la Mindanao huko Ufilipino. Katika taarifa yake Bwana Ban ametuma salamu za pole kwa serikali ya Ufilipino na familia zilizopoteza jamaa au kujeruhiwa kutokana na [...]
06/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalamun wa afya pamoja na watunga sera kutoka mataifa mbalimbali duniani pamoja na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa wameanzisha mkutano wa siku tatu nchini Tanzania kujadilia hali ya utoaji chanjo na namna ya kukabiliana na magonjwa yanayoweza kutibika kwa watoto. Mkutano huo ambao umewajumuisha wajumbe zaidi ya 600, umehusisha Shirika la idadi ya watu UNFPA [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Awamu ya pili ya chanjo dhidi ya ugonjwa wa homa ya manjano huko Darfur nchini Sudan inatarajiwa kuanza mwezi huu ili kudhibiti ugonjwa huo uliolipuka mwezi Septemba mwaka huu ambapo watu 165 wameshakufa kutokana na ugonjwa huo huku 732 wakishukiwa kuugua kwenye vitongoji 33 kati ya 64 vya jimbo la Darfur. Wizara ya afya ya [...]
06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa kwa ushirikiano na wakfu wa Rockefeller hii leo wamezindua mpango mpya ya kutambua wajibu wa wanawake kwenye vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa. Mpango huo una lengo la kuonyesha mambo yanayozishauri serikali, vyombo vya habari na umma kwa ujumla kuhusu wajibu wa [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo kwamba rais wa Syria Bashar al-Assad atawajibika kisheria iwapo serikali yake itatumia silaha za kemikali kukabiliana na upinzani nchini Syria. Bwana Ban amesema hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Baghdad, Iraq, ambako amekutana pia na Waziri Mkuu, Nuri al-Maliki. Bwana Ban amesema ameelezea [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mawasiliano ya mtandao na moja ya tovuti za shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU yalikatika kwa saa mbili na kusababisha mkanganyiko mkubwa miongoni mwa washiriki na wafuatiliaji wa mkutano wa kimataifa wa mawasiliano huko Dubai. Kukatika kwa mawasiliano ya intaneti kulisababisha washiriki na wafuatiliaji kushindwa kupata nyaraka muhimu kutoka kwenye mtandao kwa kuwa mkutano huo [...]
06/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Makubalano ya Muungano wa Afrika kuhusu usalama na misaada kwa wakimbizi wa ndani yanayojulikana pia kama makubaliano ya Kampala yameanza kutekelezwa hii leo baada ya jumla ya mataifa 15 kuyaunga mkono. Makubaliano hayo yanatoa mpangilio wa kuwalinda na kuwasaidia wakimbizi wa ndani na kuyataka mataifa ya Afrika kuzuia uhamiaji . Kamishna mkuu wa Shirika la [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Uwekezaji ulio bora kwenye kilimo ni moja ya njia madhubuti za kuangamiza njaa na na umaskini na pia kulinda mazingira. Hii ni kwa mujibu wa ripoti yenye kichwa "Hali ya chakula na kilimo mwaka 2012" iliyotolewa hii leo mjini Rome. Ripoti hiyo inasema kuwa wakulima zaidi ya bilioni moja duniani wanastahili kupewa kipaumbele katika uwekezaji [...]
06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati zimesalia siku chache tu kabla ya Siku ya Kimataifa ya Haki za Binadamu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, amesema hakuna mtu hata mmoja anayestahili kutengwa katika kufurahia haki zake, kama zilivyowekwa katika azimio la kimataifa la haki za binadamu. Bi Pillay amesema kuwa mamilioni ya watu ambao [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa, FAO limesema wastani wa bei ya chakula umeendelea kushuka ambapo kwa mwezi uliopita wa Novemba ulishuka kwa asilimia Moja nukta Tano, ikilinganishwa na mwezi uliotangulia. Ripoti ya FAO kuhusu bei za chakula inaonyesha kuwa bei ya kapu la chakula ilishuka kwa pointi Tatu na kufikia pointi [...]
06/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada na usalama kwa wapalestina, UNRWA, Filippo Grandi amekagua operesheni za shirika hilo huko Yarmouk, Syria ambako wafanyakazi 3,700 wanaendelea kutoa huduma za kijamii licha ya mzozo unaoendelea. Huduma hizo ikiwemo elimu na afya ni kwa ajili ya zaidi ya wakimbizi 500,000 wa kipalestina ambapo [...]
06/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon aliyeko ziarani Mashariki ya Kati, hii leo alitembelea Kuwait ambako ameeleza kutiwa moyo na maendeleo ya uhusiano kati ya nchi na Iraq, uhusiano ambao amesema unazidi kuimarika. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye mji mkuu wa Kuwait, Kuwait City, Bwana Ban amesema anaamini kuwa nchi mbili hizo [...]
05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limelaani shambulio la jana kwenye shule moja iliyoko karibu na mji mkuu wa Syria Damascus ambalo lilisababisha mauaji ya wanafunzi kadhaa pamoja na mwalimu mmoja. Mkurugenzi wa UNICEF kwa Ukanda wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini Maria Calivis amesema katika taarifa yake kuwa tangu kuanza [...]
05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa umesema Uwanja wa ndege wa Goma, Mashariki wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, umefunguliwa leo na unatoa huduma baada ya kufungwa kufuatia waasi wa kikundi cha M23 kuingia na kusonga ndani ya mji huo mwezi uliopita. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nesirky ametoa taarifa hiyo mbele ya waandishi wa habari [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Baraza la Usalama leo limepatiwa taarifa ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon kuhusu hali ya usalama ilivyo huko Mali Afrika Magharibi ambapo amesema hali ya usalama si nzuri na anaunga mkono mapendekezo ya Afrika kuhusu ulinzi na usalama nchini Mali. Ripoti hiyo imewasilishwa na Msaidizi wa Bwana Ban kwa masuala ya [...]
05/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za binadamu kwenye maene ya kipalestina yanayokaliwa na Israel tangu mwaka 1967 Richard Falk ametoa wito kwa Israel akiitaka itekeleze makubaliano yaliyositisha mzozo kwenye ukanda wa Gaza. Falk aliyasema hayo alipofanya ziara kwenye ukanda wa Gaza na Misri ambapo alikutana na waakilishi wa mashirika [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tatizo la uhaba wa maji katika jimbo la Darfur huko Sudan limepatiwa ufumbuzi baada ya kikundi cha pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa jimboni humo, UNAMID na benki ya Maendeleo ya Afrika, kwa ushirikiano na serikali ya Sudan kuzindua miradi kadhaa ya maji kwenye eneo hilo. Miradi hiyo yenye lengo la kukidhi [...]
05/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Kundi la Hamas chini ya uongozi wa Misri yaliyoanza kutekelezwa tarehe 21 mwezi Novemba yamewafanya wapalestina wengi kuyafikia maeneo ya uvuvi na kilimo ambayo awali hawakuwa wakiyafikia. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA linasema kuwa kulingana na ya tathmini iliyoendeshwa ni kwamba [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mpango wa kujitolea wa Umoja wa Mataifa, UNV umesema kila mwaka mamilioni ya watu duniani kote hujitolea muda wao na stadi zao kubadili maisha ya watu wengine. UNV imesema hayo leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya kujitolea ambapo msemaji wake Jennifer Stapper amesema ni fursa ya kutoa shukrani kwa wafanyakazi wa kujitolea wanaotekeleza majukumu [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Nchi nyingi, hususani zile zenye historia ndefu ya uchimbaji migodi zinaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa madhara ya madini ya risasi miongoni mwa watoto kwa kupima viwango vya uchafuzi wa madini hayo mchangani, ili kutambua ni maeneo yepi yenye hatari, na hivyo kuwaepusha watoto na maeneo hayo. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya utafiti ilochapishwa [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kampuni ya simu ya Nokia imetangaza kuunga mkono jitihada zinazoendelea kuchukuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na idadi ya watu UNFPA na kwa kuanzia kampuni hiyo ya simu imekubali kuchangia kiasi vifaa vya kujifungulia vipatavyo 3,000 ambayo yanakusudia kufanikisha uzazi salama. Uchangiaji wa huduma hiyo ni sehemu ya uungwaji mkono wa kampeni iliyoanzishwa [...]
05/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya kujitolea hii leo na kusema kuwa kazi inayofanywa na wafanyakazi wa kujitolea inasaidia kufanikisha malengo ya maendeleo ya milenia ya mwaka 2015. Katika ujumbe wake Bwana Ban amesema wafanyakazi hao wakiwemo 7,700 wa Umoja wa Mataifa wameshiriki kazi mbali [...]
05/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Rais mpya wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Mohammed Loulichki ametangaza ratiba ya shughuli za baraza hilo kwa mwezi huu ambapo amesema ulinzi na usalama kwenye ukanda wa Sahel barani Afrika ni miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaumbele. Akizungumza na waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo baada ya kuchukua wadhifa huo [...]
04/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa Ofisi ya Haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amezitaka serikali kuongeza jitihada zaidi kushughulikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu kwenye sekta ya biashara vilivyosababisha na kuendeleza mdororo wa sasa wa uchumi. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi kwenye kongamano la ngazi ya juu linaloangalia uhusiano kati ya maendeleo ya sekta [...]
04/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameonyesha wasiwasi mkubwa juu ya mpango wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu wa Korea, DPRK ya kutaka kurusha roketi kwenda anga za juu na kuitaka nchi hiyo kufikiria upya uamuzi wake ikiwemo kusitisha kabisa shughuli hiyo. Msemaji wa Bwana Ban, amemkariri Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa [...]
04/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wataalamu wa masuala ya tiba wanaendelea na mkutano wao wa siku tano huko Bonn, Ujerumani wakiangalia jinsi mionzi inavyoweza kutumika salama katika utambuzi wa magonjwa na tiba katika muongo ujao. Shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA ambalo ndilo mwenyeji wa mkutano huo linasema kuwa takribani watu Milioni Moja hunufaika na suala [...]
04/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa serikali zilizo na uwakilishi kwenye kongamano la kimataifa la kuangazia mabadiliko ya hali ya hewa, UNFCCC mjini Doha, Qatar, kudokeza mambo matano muhimu ambayo yanaweza kukelezeka. Bwana Ban amesema, kwanza, ameziomba ziafikie ahadi nyingine inayoandama mkataba wa Kyoto, ambao ndio ulio karibu sana na [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku mapigano yakizidi kuchacha nchini Syria, Kamishna msaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji UNHCR Erika Feller ametembelea eneo moja nchini Jordan linalohifadhi wakimbizi wa Syria kujionea hali jumla ya mambo. Akiwa katika kambi ya Za'atri kamishna huyo ameshuhudia namna utoaji wa huduma za kisamaria zinavyowalenga zaidi raia wasio na hatia ambayo [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Pillay ameelezea wasiwasi wake juu majaliwa ya mwanaharakati na mwanasheria Nasrin Sotoudeh ambaye hali ya afya yake imeelezwa kuzorota. Bi Sotoudeh ambaye ni mwanaharakati wa haki za binadamu yuko katika mgomo wa kula tangu Octoba 17 mwaka huu kama njia ya kupinga kuwekw agerezani na [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ombi la miaka mitatu kwa taifa la Somalia limezinduliwa humo ikiwa ndiyo mara ya kwanza uzinduzi huo kufanyika nchini Somalia. Ombi hili liliwasilishwa na naibu mratibu wa huduma za kibinadamu nchini Somalia Stefano Porretti kwa Waziri wa usalama na masuala ya ndani nchini Somalia Abdikarim Hussein Guled anayehusika na masuala ya kibinadamu. Mkakati huo kati [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa linasema kuwa linahofia usalama wa watu waliohama makwao pamoja na watoa huduma za misaada kwenye kambi zilizo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo baada ya shambulizi nje ya kambi ya Mugunga III iliyo mjini Goma siku ya Jumamosi. Msemaji wa UNHCR Adrian Edwards anasema kuwa hata [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM linashirikiana na serikali ya Ufilipino na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu kutathmini athari za kimbunga Bopha wakati huu ambapo kinaendelea kupiga eneo la Mindanao kusini mwa nchi hiyo. Kasi ya kimbunga hicho imepunguzwa kutoka Tano hadi Tatu na ripoti za awali zinaonyesha kuwepo na idadi ndogo ya waathirika. [...]
04/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kimataifa la uhamiaji, IOM, kwa kushirikiana na serikali ya Ghana imezindua tovuti yenye lengo la kuwezesha zaidi ya raia milioni Tatu wa nchi hiyo wanaoishi ughaibuni kushiriki katika maendeleo ya nchi yao. Tovuti hiyo itakuwa ni kituo kwa waghana walio ughaibuni kuweza kupata taarifa kutoka nyumbani na hata hoja zao kuweza kushughulikiwa na [...]
04/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umesema unasitisha baadhi ya shughuli zake nchini Syria pamoja na kuondoa watendaji wake ambao si lazima wawepo nchini humo kutokana na kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama. Msemaji wa umoja huo Martin Nesirky amesema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mjini New York, Marekani hii leo akikariri Idara ya Usalama [...]
03/12/2012 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwenye masuala ya watoto na mizozo ya kivita, Leila Zerrougui amesema pande zinazozona nchini Yemen zimekubaliana kuachana na mpango wa kuandikisha watoto kwenye majeshi yao. Kauli hiyo ya Zerrougui ameitoa leo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, [...]
03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO limezindua ripoti ya kuwezesha wanafunzi wenye ulemavu kupata fursa ya kutumia teknolojia ya mawasiliano na habari, ICT. Ripoti hiyo imetolewa hii leo ambayo ni siku ya watu wenye ulemavu duniani na imechapishwa katika lugha Sita, ambazo ni kiingereza, kifaransa, kispaniola, kichina, kiarabu, kirusi na [...]
03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imebainisha kuyoyoma kwa matumaini ya kukua kwa sekta ya viwanda duniani. Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya viwanda, UNIDO limetoa takwimu za sekta ya viwanda kwa robo ya tatu ya mwaka huu ambazo zinaonyesha kuwa kiwango cha ukuaji kwenye sekta hiyo kilikuwa asilimia 2.2 ikilinganishwa [...]
03/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano wa mwaka wa nchi wa wanachama wa Mkataba wa kuzuia mabomu ya kutegwa ardhini yanayolengwa binadamu umeanza huko Geneva Uswisi ambapo wawakilishi wa serikali, taasisi za kiraia pamoja na wataalamu wanajadili kwa wiki nzima na kufanyia tathmini mkataba huo ujulikanao kama Ottawa Convention. Rais wa mkutano huo Balozi Matjaz Kovacic kutoka Slovenia amesema mkutano [...]
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wa usaidizi huko Darfur, UNAMID umetia shime katika juhudi za kupambana na homa ya manjano kwenye jimbo hilo ambapo imesaidia usafirishaji wa vifaa kwenda maeneo ambako kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo inatekelezwa. Kaimu Mkuu wa UNAMID Aïchatou Mindaoudou amesema ofisi yake inajisikia [...]
03/12/2012 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mratibu Mkuu wa Masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos ametembelea Bangladesh kujionea jinsi nchi hiyo inavyojiandaa dhidi ya majanga ambapo amesema mikakati ya nchi hiyo ni mfano wa kuigwa. Bi. Amos ametaja mikakati hiyo ni pamoja na nchi hiyo kuwekeza mbinu za kujiandaa dhidi ya majanga kwa wananchi wenyewe kutokana na nchi [...]
03/12/2012 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Wakati hali inapoendelea kuwa mbaya nchini Syria kila siku wale wanaoiahama na waliosalia wote wanazidi kukumbwacha changamoto nyingi. Kuendelea kuwepo ukosefu wa usalama kumewapa wakati mgumu wahudumu wa kibinadamu wanaotoa misaada kwa watu walioathiriwa. Mratibu wa masuala ya kibinadamu nchini Syria Radhouane Nouicer anasema kuwa wanajaribu kutafuta njia za kuwafikia watu zaidi wanaohitaji misaada kulingana [...]
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuunga mkono uhuru wa kujieleza kupitia mtando wa intaneti, akiongeza kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano inazidi kubadilisha ulimwengu kwa kuwafungulia watu milango ya ufanisi, kuokoa maisha, kutoa elimu na kuwapa uwezo zaidi. Akitaja mfano wa mabadiliko ya kisiasa katika nchi [...]
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mpango wa Israel wa kujenga makazi mapya Elfu Tatu huko Jerusalem Mashariki na sehemu zingine za Ukingo wa Magharibi mwa mto Jordan umeripotiwa kumsikitisha na kumkatisha tamaa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon, na hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wake. Taarifa zaidi na Monica Morara. (SAUTI YA MONICA MORARA)
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Siku kumi na mbili baada ya waasi wa M23 kuutwaa mji wa Goma, hali ya kibinadamu na ya kiusalama bado inatia wasiwasi katika jimbo la Kivu ya Kaskazini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Takriban watu 130, 000 wamelazimika kuhama makwao na wanaishi katika kambi na makazi mengine ya dharura karibu na, au katika mji wa [...]
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema hatua zaidi zichukuliwe kutekeleza ahadi nzuri zinazotolewa kwa ajili ya kuimarisha maisha ya zaidi ya watu bilioni Moja wanaoishi na ulemavu duniani kote. Ban katika ujumbe wake wa siku ya walemavu duniani hii leo, amesema hatua hiyo ni muhimu kwa kuwa changamoto kubwa hivi sasa ni [...]
03/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezitaka nchi wanachama wa umoja huo kuongeza jitihada za kutokomeza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto huku zikihakikisha kuwa wanawake wazazi wenye virusi vya Ukimwi wanaishi na afya zao zinastawi. Bwana Ban amesema hayo katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku ya Ukimwi [...]
01/12/2012 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »