Zaidi ya watu milioni 7.7 wameathiriwa na mafuriko Nigeria

Kusikiliza /

mafuriko Nigeria

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yamesema mafuriko nchini Nigeria yameathiri zaidi ya watu milioni 7.7. Mafuriko hayo ambayo yameelezewa kuwa mabaya zaidi katika kipindi cha miaka 40, yamesemekana kuwaua zaidi ya watu mia tatu, huku wengine zaidi ya milioni mbili wakiwa wamejiandikisha kama wakimbizi wa ndani.

Shirika la Afya Duniani, WHO limesema visa vya maambukizi ya ugonjwa wa malaria vimeongezeka kutokana na mafuriko hayo, ingawa hakuna mlipuko mkubwa ulioripotiwa. WHO pia imeeleza uharibifu uliofanyika dhidi ya majengo na vifaa vya afya katika maeneo yaloathirika.

Nalo Shirika la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limesema maeneo yaloathirika hayana huduma za maji safi, kwani asilimia 63 ya maji ya kunywa na kupikia hutoka kwenye mito na visima vilivyo wazi.

Afisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA limesema ingawa mafuriko hayo yanapungua, mashirika ya kibinadamu yanakadiria kuwa gharama ya mahitaji ya kibinadamu ni dola milioni 38, hasa katika majimbo 14 yaliyoathirika zaidi. Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA JENS LEARKE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031