Zaidi ya raia 350,000 wa Haiti bado wanaendelea kuishi kwenye makambi

Kusikiliza /

makambi nchini Haiti

Idadi ya raia walioathiriwa na tetemeko la ardhi liliikumba Haiti miaka mitatu iliyopita,ambao bado wanaendelea kuishi kwenye makambi inakadiriwa kufikia 357,785 ikiwa imepungua kwa wastani wa asilimia 70 ikilinganishwa na takwimu za awali.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM Gregoire Goodste anasema kuwa kiwango hicho ni hadi kufikia mwezi Octoba mwaka huu, na imepungua kutoka watu 1,536,477 walioandikishwa July 2010.

IOM inakusudia kushirikiana na mashirika ya kim ataifa ili kukusanya kiasi cha dola za kimarekani 800,000 ili kufanikisha miradi ya kuwakirimu wahanga hao katika msimu wa mwaka 2013. Taarifa zaidi na George Njogopa.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031