WHO yatabiri kuendelea kuongezeka kwa wagonjwa wa Kisukari duniani

Kusikiliza /

ugonjwa wa kisukari

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na ugonjwa wa Kisukari, Shirika la afya duniani linasema kuwa watu Milioni 347 duniani kote wanasumbuliwa na aina ya kwanza ya ugonjwa wa kisukari.

WHO imesema mwaka 2004 watu Milioni 3.4 walikufa kutokana na ugonjwa wa kisukari ambapo zaidi ya asilimia 80 ya vifo hivyo ni katika nchi zenye vipato vya chini na kati.

WHO imesema kuwa kiwango cha vifo kitaongezeka kwa theluthi mbili hadi mwaka 2030 kulingana na makadirio ya mwaka 2008. Tarik Jasarevic ni msemaji wa WHO:

"Ni ugonjwa sugu lakini unaweza kupunguzwa sana kwa kuwa na mfumo sahihi wa maisha na kupunguza matumizi ya pombe, kuacha kuvuta sigara, kupata lishe bora na mazoezi. Kwa hiyo ni tatizo linaloongezeka na nchi zinatambua."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031