WHO yahitaji dola Milioni 10 kukidhi huduma ya tiba huko Gaza

Kusikiliza /

watoto Gaza

Shirika la afya duniani, WHO linaomba dola Milioni Kumi kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba na dawa za kutumika kwenye vituo vya afya huko Ukanda wa Gaza ambako idadi ya wagonjwa imeongezeka kutokana na mapigano yanayoendelea huku vituo vya afya vikiripotiwa kushambuliwa.

Mkuu wa ofisi ya WHO huko Gaza Dkt, Mahmoud Daher ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kuwa tangu kuanza kwa mapigano hayo tarehe 14 mwezi huu watu 132 wameuawa na wengine zaidi ya Elfu Moja wamejeruhiwa ambapo kati yao waliouawa 30 ni watoto na 11 ni wanawake.

Dkt. Daher amesema kutokana na ongezeko kubwa la wagonjwa, mfumo wa afya kwenye eneo hilo unashindwa kukidhi mahitaji ambapo hospitali zinalazimika kuwaondoa wagonjwa wa kawaida ili kuhudumia majeruhi wa mapigano hayo huku vifaa tiba na dawa vikiwa hazitoshelezi licha ya kwamba wahudumu wa afya kwa sasa siyo tatizo.

(SAUTI YA DKT. DAHER)

"Uhaba wa vifaa na madawa ndio tatizo kubwa kwa kuwa zaidi ya asilimia 50 ya dawa muhimu zitatosha kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja. Na katika mazingira ya sasa matumizi yanazidi na hivyo dawa zinamalizika haraka. Hivyo uwezo wa kuhudumia wagonjwa kadri wanavyoongezeka itakuwa ni tatizo kama ambavyo imeshuhudiwa katika siku chache zilizopita. Tumetoa taarifa wa jumuiya ya kimataifa itusaidie dola Milioni Kumi lakini hadi sasa mwitikio ni mdogo".

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031