WFP yashukuru Lebanon kwa kusaidia wakimbizi wa Syria

Kusikiliza /

Ertharin Cousin

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani, WFP Ertharin Cousin, amehitimisha ziara yake nchini Lebanon na kuipongeza serikali ya nchi hiyo na wananchi wake kwa kuwasaidia wakimbizi kutoka Syria wanaotafuta hifadhi salama.

Bi. Cousin ambaye amewaeleza waandishi wa habari mjini Beirut kuwa kitendo hicho cha serikali ya Lebanon kinarahisisha kazi ya WFP ya kusaidia wakimbizi hao.

Amesema wakati wa ziara hiyo alikuwa na mazungumzo na Rais wa Lebanon Michel Suleiman na Waziri Mkuu Najib Mikati kuhusu changamoto zinazokabili nchi hiyo kuhudumia wakimbizi hao pamoja na hatua zinazochukuliwa na WFP na washirika wake.

Halikadhalika alipata fursa ya kuzungumza na wakimbizi hao ambao walimweleza madhila yao ikiwemo kukimbia nchi yao bila vifaa muhimu na hivyo wajibu wake ni kusaidia kupaza sauti juu ya mahitaji yao.

Mkuu huyo wa WFP amesema atashirikiana na jumuiya ya kimataifa kuhakikisha wanaendelea kushughulikia mahitaji muhimu ya raia wa Syria walio ndani ya nchi yao na hata nchi jirani.

Ziara ya Bi. Cousin nchini Lebanon ni kituo cha kwanza katika maeneo atakayotembelea kwa siku Tatu Mashariki ya Kati kujionea hali halisi ya wakimbizi wa Syria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031