Wataalam wa UM kukagua hatua za serikali ya Tunisia kuendeleza haki

Kusikiliza /

Pablo de Greiff

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa, Pablo de Greiff, ataizuru Tunisia tokea kesho Novemba 10 hadi 16, ili kufuatilia hatua zilizochukuliwa na serikali kuhusu ukiukaji wa haki za binadamu zamani na kuendeleza mfumo wa haki baada ya mabadiliko.

Ziara hiyo ndiyo ya kwanza kufanywa na mtaalam huru ambaye ameteuliwa na Baraza la Haki za Binadam la Umoja wa Mataifa, ili kukagua na kushauri kuhusu kuendeleza ukweli, haki, marekebisho na kuhakikisha kutorudiwa kwa matukio ya zamani.

Amesema Tunisia ipo katika nafasi ya kuondoka kwenye unyanyasaji na ufisadi na kuwa jamii inayoongozwa kisheria. George Njogopa na taarifa kamili.

(SAUTI YA GEORGE NJOGOPA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031