Waandishi wa habari wanawake Mauritania wapatiwa mafunzo kwa msaada wa UNESCO

Kusikiliza /

UNESCO, IPDC

Nchini Mauritania, waandishi wa habari wanawake kutoka radio, magazeti na wale wanaochapisha habari kwenye intaneti v wamepatiwa mafunzo kuhusu maadili na kanuni za uandishi wa habari.

Mafunzo hayo ya siku nne yaliyoendeshwa na programu ya kimataifa ya kuendeleza mawasiliano, IPDC kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, yalilenga kujenga uwezo wa waandishi hao wa habari katika stadi za taaluma hiyo.

UNESCO imesema hatua ya kutoa mafunzo kwa wanawake hao ambao ni wanachama wa chama cha waandishi wa habari wanawake nchini Mauritania inatokana na suala kwamba wanawake mara nyingi hukosa fursa za mafunzo katika vyombo vya habari wanavyofanyia kazi.

Wakufunzi walitoka Morocco na Mauritania ambapo mafunzo hayo yalitoa fursa kwa washiriki kubadilishana taarifa kuhusu mabadiliko katika tasni ya habari kwenye nchi mbili hizo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930