Utafiti mpya wa UNCTAD wazingatia sera za kibiashara na usawa wa kijinsia katika nchi tatu

Kusikiliza /

nembo ya UNCTAD

Sera za kibiashara huathiri kwa njia tofauti sehemu mbali mbali za jamii, kama vile wanaume na wanawake, wakaazi wa vijijini na mijini, watu tajiri na maskini. Hayo ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Kamati ya Umoja wa Mataifa kuhusu Biashara na Maendeleo, UNCTAD, wa hali katika nchi za Cape Verde, the Gambia na Lesotho.

Ripoti ya utafiti huo, yenye kichwa, Sera za Kibiashara na usawa wa kijinsia, inaangazia athari za kijinsia za biashara katika kila nchi, na inatarajiwa kunachangia ukusanyaji maoni kuhusu jinsi ya kuangazia masuala ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Wakati tarehe hiyo ya kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ikiwa inakaribia, Umoja wa Mataifa ulianzisha harakati za kuweka mkakati wa maendeleo baada ya mwaka huo wa 2015, na ukusanyaji maoni kwa ngazi ya kimataifa umeanza, ukizingatia masuala tisa muhimu, na ambayo mojawapo ni suala la usawa wa jinsia. Alice Kariuki na taarifa kamili.

(SAUTI YA ALICE KARIUKI)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031