UNRWA yaeleza wasiwasi juu mashambulio dhidi ya wakimbizi wa kipalestina

Kusikiliza /

nembo ya UNRWA

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada na ulinzi kwa wakimbizi wa kipalestina, UNRWA imezieleza mamlaka ya Syria juu ya hofu yake kuu kwa madhara wanayopata wakimbizi wa kipalestina kutokana na mgogoro unaoendelea nchini humo.

Hofu hiyo inafuatia mauaji ya Jumatatu ya Dkt. Rehab Awadallah, mwalimu wa UNRWA nchini Syria pamoja na mpwa wake mpalestina yaliyotokana na shambulio wakati wakitembea kwenye eneo la Yaamanouk, ambalo ni makazi ya raia wa Syria na wakimbizi wa kipalestina.

Taarifa ya UNRWA imesema tukio hilo ni la tano la mauaji linalotokana na mzozo unaoendelea nchini Syria na kwamba Ofisi hiyo inataka pande zote zinazozozana kujiepusha kushambulia maeneo ya raia. Badala yake imezitaka zizingatie wajibu wao kwa mujibu wa sheria za kimataifa ili kulinda wakimbizi wa kipalestina na raia wengine dhidi ya mzozo huo.

Halikadhalika UNRWA imezitaka pande hizo nchini Syria kumaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo na mashauriano

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031