UNICEF yaelezea wasiwasi kuhusu elimu na afya ya watoto mashariki mwa DRC

Kusikiliza /

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa karibu wakimbizi wa ndani 140,000 wanaishi kwenye shule tatu za umma, kituo cha Don Bosco na kwa kambi tatu za wakimbizi wa ndani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo. UNICEF inasema kuwa watoto wako kwenye hatari ya maradhi ya kuambukiza yakiwemo kipindupindu kutokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa. Marixie Mercado ni msemaji wa UNICEF

SAUTI YA Marixie Mercado

Kuna idadi kubwa ya watoto wanosomba maji kutoka ziwa Kivu hali inyoongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa. Tunafahamu karibu visa 115 vya watoto waliotengwa na familia zao lakini makadirio yanaonyesha kuwa huenda idaihiyo ikawa ya juu. Idadi ya waasi wa M23 imeongezeka siku chache zilizopita na kuna makundi mengine yaliyojihami yanaoendesha shghuli zao eneo hilo na kungozea uwezakano wa kuwaajiri watoto.

Shirika la afya duniani WHO linasema kuwa huku mapigano yakiwa yamechacha kuna changamoto kubwa kwa waliojeruhiwa kupata matibabu huku ripoti zaidi zikisema kuwa baadhi ya vituo vya kiafya vimeporwa

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031