UNHCR yaipongeza Philippines kwa kuanzisha mpango unaowajali wakimbizi

Kusikiliza /

wakimbizi wa Ufilipino

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limepongeza serikali ya Philippines kwa kuwa nchi ya kwanza katika eneo la Asia-Pasifik kuanzisha mpango wenye shabaha ya kuwalinda wakimbizi na jamii ya watu wasiokuwa na ukazi maalumu.

Idara ya haki na sheria ya Philipenes hivi karibuni ilichapisha mwongozo ambao pamoja na mambo mengine umekusudia kuboresha mifumo ya utambuzi hadhi ya wakimbizi na kuongeza kipengele ambacho kinatambulisha jamii ya watu wasiokuwa na ukazi maalumu.

Mwongozo huo mpya unaanza kufanya kazi kuanzia leo ni sehemu ya utekelezwaji wa maazimio ya kimataifa kama ilivyoanishwa kwenye itifaki ya kimataifa ya mwaka 1954.

Maafisa wa UNHCR wamesema kuwa hatua hiyo iliyochukuliwa na serikali ya Philippines inaonyesha namna taifa hilo linavyothamini na kuzingatia mahitaji ya usamaria mwema.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031