UNESCO yataka mauaji ya waandishi wa habari Somalia yachunguzwe

Kusikiliza /

vyombo vya waandishi habari

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, ameelezea kusikitishwa kwake kuhusu usalama wa waandishi habari nchini Somalia, na kutaka uchunguzi ufanywe kufuatia mauaji ya Mohammed Mohamud Tuuryare na Ahmed Farah Ilyas mnamo Oktoba 28 na Oktoba 23 mfululizo.

Bi Bokova amelaani mauaji hayo, na kusema kuwa idadi ya waandishi habari ambao wameuawa nchini humo inatia hofu. Amesema kuwa anahofia uwezo wa waandishi wa habari kutekeleza kazi zao katika mazingira ya ghasia kama yaliyoko nchini Somalia, huku akipongeza ujasiri wao.

Ametaka serikali ichunguze uhalifu huo, ambao amesema unaiathiri jamii nzima, kwani unadunisha uhuru wa wananchi wa kujieleza, ambao ni haki ya kimsingi, na uwezo wao kupokea habari wanazohitaji.

Mauaji ya wawili hao katika kipindi cha wiki moja yamefanya idadi ya waandishi wa habari waliouawa nchini Somalia mwaka huu pekee kufikia 17.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031