Umoja wa Mataifa waadhimisha siku ya falsafa duniani

Kusikiliza /

 

Siku ya Falsafa Duniani

Leo ni siku ya falsafa duniani, siku inayosherekewa na Shirika la elimu , Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO kila tarehe 15 mwezi Novemba. Kauli mbiu ya siku ya mwaka huu ni "vizazi vijavyo". Kwenye makao makuu mjini Paris UNESCO inatarajiwa kupanga majadiliano kuhusu vizazi vijavyo na vijana.

Vizazi vijavyo ndiyo itakuwa agenda kuu kwenye siku ya kimataifa ya falsafa ya mwaka 2012 wakati ulimwengu unapokabiliana na matokeo ya mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu maendeleo endelevu wa Rio+20. UNESCO pia inatarajiwa kuongoza matukio yanayoleta pamoja masuala haya yote ambapo kundi la watoto wa shule kutoka mjini Paris litaweka mabango yatakayosomwa na watoto wenzao. Matukio kadha pia yanatarajiwa kuandali sehemu mbali mbali za ulimwengu kungazia hasa kuhusu vizazi vijavyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031