UM yapongeza kuundwa kwa serikali mpya nchini Libya na kusisitiza mashauriano

Kusikiliza /

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa UM nchini Libya, Tarek Mitri.

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Tarek Mitri amempongeza Waziri Mkuu wa Libya Ali Zeidan na baraza lake la mawaziri kufuatia kuundwa kwa serikali mpya nchini humo.

Mitri, katika taarifa iliyotolewa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kusaidia Libya, UNSMIL amelipongeza pia bunge la Libya kwa kuidhinisha serikali hiyo na kuitakia mafanikio wakati wa kushughulikia changamoto zinazokabili nchi hiyo ikiwemo kujenga taasisi za ulinzi na usalama, kuendeleza maridhiano ya kitaifa na kusimamia utawala wa kisheria.

Hata hivyo Mitri amesema katika kukabiliana na changamoto hizo, serikali hiyo inawahitaji wananchi waLibyana kuwataka wananchi wote kushiriki kuleta maridhiano ya kitaifa na kuimarisha taasisi za kiraia na zile za kiusalama nchini humo.

Taarifa hiyo imemkariri Mwakilishi huyo maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akisema kuwa Umoja wa Mataifa utashirikiana na serikali mpya yaLibyana wananchi wake kwa mujibu wa azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililopitishwa mwezi Machi mwaka huu.

Azimio hilo liliongeza muda wa UNSMIL ili kusaidia Libya katika kipindi hiki cha mpito cha kuunda taifa la kidemokrasia.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031