UM wataka China kushughulikia masuala ya haki za binadamu huko Tibet

Kusikiliza /

Navi Pillay

Umoja wa Mataifa umeitaka China kushughulikia haraka iwezekanavyo vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vinavyochochea maandamano na vurugu huko Tibet ikiwemo watu kujiua kwa kujichoma moto.

Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay amesema tangu mwaka 2011 kumekuwepo na matukio zaidi ya 60 ya watu kujiua kwa kujichoma moto na kwamba ana wasiwasi juu ya madai ya kuendelea kuwepo kwa ghasia na vitendo vya utesaji dhidi ya watu wa Tibet wanaotaka kutekeleza haki yao ya msingi ya kujieleza, kutangamana na kuabudu.

Bi. Pillay ametaka serikali ya China kuruhusu kundi huru la watu wasioegemea upande wowote kutembelea maeneo ya Tibet kutathmini viwango vya haki za binadamu na wakati huo huo iondoe kizuizi dhidi ya vyombo vya habari kufika maeneo hayo.

Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa.

"Bi. Pillay pia ametoa wito wa kuachiwa huru kwa watu wote wanaoshikiliwa kwa kushiriki katika mikusanyiko ya amani huko Tibet. Pia anataka wakazi wa Tibet kujiepusha na aina yoyote ile ya vitendo au vurugu za kupindukia kama vile kujiua kwa kujichoma moto na amezita jumuiya na viongozi wa kidini kutumia ushawishi wao kuzuia aina hiyo ya kujiua. Bi. Pillay anatambua jinsi ambavyo wakazi wa Tibet walivyochanganyikiwa na kukata tamaa, hali ambayo inawasukuma wachukue hatua hiyo. Hata hivyo amesema kuna njia nyingine ya kuonyesha hisia zao kwa dhati. Ni muhimu serikali nayo ikatambua hilo na kuruhusu watibeti kuonyesha hisia zao bila hofu ya kuwepo kwa kisasi."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031