Uhaba wa mashine za kupumulia wasababisha vifo vya watoto Syria: UNICEF

Watoto nchini Syria

Umoja wa Mataifa umesema idadi kubwa ya watoto wachanga nchini Syria wanafariki dunia kutokana na uhaba wa mashine za kuwawezesha kupumua pindi wanapozaliwa kabla ya wakati.

Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema jopo la wataalamu wake lilitembelea jimbo la Al Raqqah nchini Syria ambapo hospitali kuu ya eneo hilo ina mashine 14 tu ya kuwezesha watoto kupumua wakati idadi inayohitajika ni zaidi ya 60.

Wataalamu hao walipata fursa ya kuzungumza na wahudumu wa afya ambao walisema kuna matukio mengi ya wanawake kujifunga kabla ya wakati na hata mimba kuharibika.

Msemaji wa UNICEF Marixie Mercado ameeleza kuwa kutokana na maisha magumu, wanawake wameamua kuwavalisha watoto wao mifuko ya nailoni badala ya nepi za kawaida.

(SAUTI YA MARIXIE MERCADO)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930