Uhaba wa chakula washuhudiwa kwenye nchi za kusini mwa Afrika

Kusikiliza /

njaa kusini mwa Afrika

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasema kuwa zaidi ya watu milioni 3.5 walio nchini Malawi, Zimbabwe na Lesotho wanahitaji msaada wa chakula kwa muda wa miezi minne ijayo wanapongojea msimu wa mavuno.

Kiasi kidogo cha mvua maeneo ya kusini mwa Afrika kimesabisha kushuhudiwa uhaba wa chakula kwenye nchi hizo tatu huku mahitaji yakitarajiwa kuongezeka katika ya msimu wa upanzi ambao ni mwezi Oktoba na Novemba na wa kuvuna mwaka ujao.

Bei ya mahindi imeongezeka kwa asilimia 60 kwenye masoko nchini Lesotho tangu mwanzo wa mwaka . Nchini Malawi nako bei ya mahindi imepanda kwa silimia 80 tangu wakati kama huu mwaka uliopita. WFP inasema kuwa kupitia usaidizi wa serikali , wahisani na mashirika mengine inakusanya misaada kuwasaidia walio na mahitaji zaidi. Elizabeth Byrs, ni msemaji wa WFP.

(SAUTI YA ELIZABETH BRYS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2016
T N T K J M P
« sep    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31